Bibi zetu walipanda chikichi hazikuwatoe je sisi zitatutoa kama mifumo ni ileile ya mabibi.Hata processing ni vivilevile.
Binafsi nilitaka kupanda chikichi kwetu kigoma,nikazama kusoma articles zinazohusu chikichi, nyumbani Tz hakuna tafiti zozote, nyingi nilizipata kutoka Asia, Singapore, Thailand, Vietnam nk.
Mambo makubwa niliyoyapata ni kwamba chikichi ni zao ka kiviwanda hata biofuel ni zao mojawapo, wenzetu kunaviwanda vinatumia mawese kuendesha mitambi yao.
Vyakula vingi ulaya wanavitengeneza na mawese. Nk, nk
Nilipochunguza hapa home nikagundua mawese yanatumika zaidi kwa sabuni na mafuta ya kula kidogo.Products nyingi za mawese zinatupwa kuanzia makanfi(lugha ya kigoma kambakamba baada ya kuchuja), maganda ya mise, chelewa,majani.
Bei ya mawese lita haizidi sh1500 kulinganisha na mafuta mengine.
Binafsi nilitupiliambali wazo la mawese nikaamua kununua mashamba ya kupanda Parachichi.
Parachichi unauza ghafi shambani chikichi una hudumia shamba, una vuna ngazi, unapeleka nyumbani,unavundika,unakamua unapeleka sokoni nk. Mkulima wa parachichi Alishasahau anasubiri mavuno ya pili were unahangaika .Chikichi kila siku upo shamba kuhudumia shamba.
Mambo ni mengi sana, mkigoma bora aanze kupanda korosho,ndizi,kahawa, parachichi,maharage,afuge samaki chikichi ziwe za mwisho.
Wanakigoma tusipochekecha akili tutaendelea kuwa masikini, wanasiasa wana ajenda zao nawe mkulima weka ajenda zako za kuutokomeza
umasikini.Kigoma ni mkoa wenye fursa nyingi Ila umedumaa hata wakazi wake hawana siha wala furaha ya maisha.Binafsi huwa naumia sana kuuona mkowa wetu ukiwa wa mwisho kimaendeleo.
Kupanga ni kuchagua, chxgua kuendelea kuwa masikini au kuutokomeza umasikini.Kamwe mwanasiasa hawezi kuutokomeza umasikini Bali ni were mwenyewe.Chagua zao la kukutoa ktk umasikini na so zao la kuwasaidia wanasiasa kudhibi mfumuko wa bei za mafuta.Kigoma muwe na akili za demand and supply,sio mtu anawaambia tu pandeni nanyi mnakulupuka bila kutafiti.
Siku mkiuza Lita sh 500 msije kumlaumu mtu, kigoma itainuliwa na watu wenye akili timamu.