Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini inahitajika ULINZI mkuu? Kuna uwezekano wa kuibiwa? Mkuu tupe fact kidogo kuhusiana na hii issue.Vanilla inahitaji maji ya wastani,kivuli , mbolea, wakati wa pollination mtu awepo shambani kuoanisha.. Ua lisipohudumiwa ndani ya saa 5 imekula kwako. Zikisha komaa ulinzi 24/7 ni muhimu tena ulinzi madhubuti sio wa virungu na panga.
Huko Madagascar inauzwa hadi usd180 kwa nini huku kwetu iuzwe bei rahisi hivi???Yaani kama unaamua kulima kisa umesikia vanila kilo 1M siku ukifika sokoni ndiyo unagundua balaa ulilolivaa.
Hata hivyo kwa maoni yangu 30K kwa kilo bado ni fair unlike mahindi.
Hivi biashara ya maua bado inalipa?Zao hili linazidi maua???
Mkuu uki google utapata picha kamili zaidi.Tuonyesheni hata picha ya hiyo vanila
"Upinzani umetucherewesha sana"Tumechelewa Sana Ndugu Zangu 😀😂😁😃
Kuna mdau kakupa jibu sababu ni grade na Madagascar wanaiuza ikiwa imeshasindikwaHuko Madagascar inauzwa hadi usd180 kwa nini huku kwetu iuzwe bei rahisi hivi???
Hiyo inafanywa na ma tycoon tu mkuu.Kama bei iko juu ni kwa nini Madagaska ni taifa maskini kiasi hicho??
Oho hapo kwenye kusindika ndo hatua zake zipoje sasa mkuu.. Mimi nikajua inakaushwa tu juani maana ukiwa kavu ndo bei inakuwa juu..Kuna mdau kakupa jibu sababu ni grade na Madagascar wanaiuza ikiwa imeshasindikwa
Dah unajua mkuu nilishawishika sana na kwa madai yao wewe ndo unaingia cost zote hadi kuvunwa ni miezi mitatu tu then wao wanakupa shamba na soko wanakutafutia. Kumbe ground mambo ni tofauti kabisa mkuu..Kaka zile ni hadithi tu za wale jamaa wa njombe kwanza amna vanilla inayokomaa kwa muda wa miezi mitatu isipokuwa vanila huanza kuchavushwa maua kuanzia mwezi wa sita toka kupandwa na pollination yake ni mkono amna wadudu wala upepo ni wewe unahamisha mbegu kwa maua yaani ni hand pollination.
Lingine ni kuwa Vanilla huwa ikiwa mbichi ili kuwa vanila kavu kuna usindikaji hufanyika na kisha kuanikwa, vanilla hupitia usindikaji ili upate kavu na kuna vigezo vyake.
Vanila huchumwa shambani kwa vigezo pia ukikosea kuchuma au ukapitiliza muda unapata low grade. Vanila mbichi ni ile ambayo haijasindikwa na huuzwa kwa grade.
Hapa Tanzania sehemu kama bukoba wanunuzi wengi hununua vanila mbichi sababu wanasindika kwa vigezo vyao wanavovitaka.
Madagascar unaweza kuexport vanila kavu ukapata soko kirahisi.
Kwenye Swala la bei ya Vanilla kilo moja siyo Milioni moja na hata nje hiyo bei haijafika, Japo ni kweli Vanilla iliwahi kuuzwa Shilingi milioni moja na zaidi kwa kilo kwa madagascar tu mwaka 2019 nadhani ilihadimika. Kwa Tanzania vanila kavu iliuzwa shilingi laki 4 mpaka 6 kwa kilo mwaka 2019 na Uganda walinunua sana laki 4 kwa kilo kule bukoba.
Hawa jamaa wa njombe wanawachota watu akili kwamba walimiwe inaweza rudi tena kama 2019 wanaishi kwa historia na siyo reality ya sasa kilo ni 30K kwa bukoba vanila mbichi anaye bisha na abishe.
Vanilla haijawahi kuuzwa Shilingi milioni moja hapa bongo believe it or leave it.
Asante sana boss ..nasubiri PM yako mkuu..Karibu, nitaku-PM kukuelekeza nilipo
Mimi sijui kitu kuhusu vanila na nafikiri unasoma kwa kuruka majibu ila majibu yapo juu hapo.Oho hapo kwenye kusindika ndo hatua zake zipoje sasa mkuu.. Mimi nikajua inakaushwa tu juani maana ukiwa kavu ndo bei inakuwa juu..
Watu kuna kitu kinawapa wasi wasi kuhusu bei yake.Kama bei iko juu ni kwa nini Madagaska ni taifa maskini kiasi hicho??
Mkuu tatizo ya hili zao hapa Tanzania wengi hasa kule bukoba wanalima na kufika hatua ya uvunaji, wafanyabiashara au niseme kampuni zinapenda kununua Vanila mbichi na wao wanaenda kukausha kwa viwango wanavotaka wao.Oho hapo kwenye kusindika ndo hatua zake zipoje sasa mkuu.. Mimi nikajua inakaushwa tu juani maana ukiwa kavu ndo bei inakuwa juu..
Aha kumbe kuna namna ya kukausha ..nikajua inaekwa tu juani ina kauka..Mkuu tatizo ya hili zao hapa Tanzania wengi hasa kule bukoba wanalima na kufika hatua ya uvunaji, wafanyabiashara au niseme kampuni zinapenda kununua Vanila mbichi na wao wanaenda kukausha kwa viwango wanavotaka wao.
Vanila ukiona inafaa kukausha unaweza ukafanya hivo ila utafanya usindikaji hapa kuna hatua kama kuichemsha vanila kwa Temperature fulani ukitumia Thermometer ili ikifika limit inayotakiwa unastop zoezi. Endapo utasindika vibaya na utakausha vibaya hutopata taste ya vanila inayohitajika hivyo vanila yako itaharibika na hutoweza kuuza. Na kwa sababu vanila hutumika kwa matumizi mbali mbali kama keki, kuongeza ladha ya vyakula na vinywaji, manukato na mafuta, n.k hivyo ni lazima vanila iwe na ukavu unaotakiwa.
Huu hapa mfano wa Vanila kavu
View attachment 1906165
Kukausha peke yako inakuwa risk sana waweza kukosa soko kwa sababu ya bei mkuu?!Bukoba hawakaushi kwa sababu wengi wanaogopa wezi. ikikomaa anauza kwa bei ya shambani, hakuna kubeba risk.
Linahitaji nguvukazi na muda mwingi sana kulihudumia, hiyo kilo moja kuipata si mchezo. Kiufupi lina bei kubwa ila faida ni ndogo sanaGharama za kulima vanila zipo juu mno. Achana nalo litakufilisi.