Zari amvua hirizi Tiffah

Zari amvua hirizi Tiffah

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Zarinah Hassan a .k .a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ?hirizi?, hali iliyowafanya watu wengi wabaki na vingi viulizo .

Mtoto wa staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platinumz, Tiffah .

Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo .

Hata hivyo , wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ?hirizi? hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina , Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.

Baada ya Tiffah kudumu na ?dawa ? hiyo kwa miezi michache ( kitu ambacho si cha kawaida ), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ?hirizi? hiyo .

Tiffah akiwa na wazazi wake .

Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ?hirizi? hiyo na nyingine hana .

Kufuatia uamuzi huo , baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa .

Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake , alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo hayo hayapo . Kitendo cha yeye kwenda Sauzi na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau , amemdharau Diamond na mama yake pia , siyo sawa ,? alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam .

Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo
 

Attachments

  • 1446969357612.jpg
    1446969357612.jpg
    72.5 KB · Views: 2,774
Ile nasikia wanavaa miezi miwili tu maana hata mtoto wa esma naye alivaa mda mchache kama tiffa tu hawajavaa km uswahilin mpaka miaka mitatu
 
Ile nasikia wanavaa miezi miwili tu maana hata mtoto wa esma naye alivaa mda mchache kama tiffa tu hawajavaa km uswahilin mpaka miaka mitatu

Mwenye baba kaitoa
 
safi zari. Ni ujinga tu. Ina maana mtoto asipovaa akui au?
 
Imani Mbovu Mikamba Meusi ni ujinga kumfunga mtoto.
 
Akuna cha utamaduni hizo no local believes mbona si watoto wote wanaovalishwa na wanakua vizuri
Ila hatuwezi jua mambo ya watu ndani
 
Mambo ya kichawichawi tu,hilizi hazina nafasi kwenye karne ya 21,watu wanakimbizana na sayansi sasa sio uchawi.Hata Mimi nilikuwa namshangaa diamond yaani super staa kabisa mtoto wake anavaa hilizi?
 
Kumvisha mtoto hirizi ni ujinga mkubwa kwani hivyo vitu vilifanywa na watu wa zamani kwa kutofahamu lkn sasa hivi mtu huwezi kumvisha huo uchafu mtoto wako ni sawa na kumkabizi shetani mtoto wako.

Big up Zari.
 
Ni sawa na kumbatiza au kumsomea maulidi mtoto ni ufala tu. Haisaidii kitu chochote.
 
Kama kweli walimvalisha hirizi, basi safi sana.

Imani za kishirikina ni kilele cha ujuha.
 
Sijui kama watu humu wameshirikisha akili zao kulijadili, ila hiko hivii kile kitambaa kavishwa na mama yake DIAMOND a.k.a Bibi Tiffah na ni katika kanuni zao huwa kila mtt anayezaliwa anavishwa hadi akitimiza miezi 2 na yule Tiffah keshatimiza miezi 2 ndo mana Zari kamvua si kwa maamuzi yake ila muda wake wa kukivaa kile kitambaa umeshakwisha na si vinginevyo huu ndo ukweli. Bahati mbaya tu picha za Bibi wa Bibi wa Bibi wa DIAMOND na Mama wa DIAMOND za miezi miwili hazipo nao mungewaona wameveshwa hiyo kitu.
 
Tanzania tuna uhuru wa kuabudu/imani. Kama mtu anaamini mizimu ya kwao mi sioni tatizo alimradi avunji sheria. Nyinyi mnaowavesha watoto zenu rosali ndio mnajiona mpo sawa Sana? Au kwasababu zimeletwa na wazungu?
 
Rozari zinafaa kwa kuwa ni product ya muzungu teh teh teh
 
Back
Top Bottom