lukelo sakafu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 2,938
- 517
mkuu umetumwa na mond?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaan wema kazimwaa magazeti yote ni zariii
Zari kwao ma paparazi wanampenda sana pia, so msishangae wa nchini kwetu...ukiwa na nyota ni nyota tubila jitihada nyingi hata ukitulia bila kuongea neno watakusaka na kukutaka habari zako. Zari yupo juu
Uongo mweusi, Zari hajaenda kuhudhuria msibani kama unavyopenda tuamini, kajipange upya!!!
Nitamwambia akupe wewe, tumlee
Yaan wema kazimwaa magazeti yote ni zariii
Zari kwao ma paparazi wanampenda sana pia, so msishangae wa nchini kwetu...ukiwa na nyota ni nyota tubila jitihada nyingi hata ukitulia bila kuongea neno watakusaka na kukutaka habari zako. Zari yupo juu
Alienda morogoro bwana, ni kweli
Hakuna lolote, ashukuru kuwa na Diamond, kabla ya hapo nilikuwa hata simjui
Nimekumic kumamae
Kazi ipo! Mwandani wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond Platnumz, Zarinah Hassan Zari juzikati alizua kizaazaa kisa ujauzito alipohudhuria kwenye msiba wa aliyekuwa bosi wa Tip Top Connection, Abdul Taletale Abdul Bonge aliyefariki dunia ghafla wikiendi iliyopita. Tukio hilo la Zari lilichukua nafasi katika Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo mkoani hapa ambapo mastaa kibao walisafiri kutoka Dar kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo.
ILIKUWAJE?
Awali, katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa mapema Jumanne wiki hii, Zari na Diamond, wakiwa wameongozana na wapambe wao walifika eneo la msiba ambapo kwa taratibu za Kiislam, wanawake hawachanganyiki na wanaume hivyo Zari akachukuliwa kwenda upande mwingine huku Diamond akielekea upande wa wanaume.
HALI YA HEWA YABADILIKA
Mara baada ya mastaa hao kutinga eneo hilo, umati mkubwa uliokuwa msibani hapo ulianza kuwazingira huku kila mmoja akitaka kuwaona.
ZARI AIBUA KIZAAZAA
Akiwa upande wa wanawake wenzake, Zari alijikuta akizungukwa na baadhi ya watu walionekana wazi kumchunguza kuanzia miguuni hadi kichwani ikidaiwa kuwa, walikuwa wakicheki kama kweli ana mimba ya Diamond.
Mwee, huyu ndiye Zari wa Diamond! Hivi mimba anayo kweli au ndiyo haya mambo ya mastaa wetu, mhh lakini kweli kitumbo kama kimetuna vile, alisikika akisema mmoja wa wanawake hao.Uwepo wa mwanadada huyo uliwafanya wengi kusahau ishu ya msiba na kujikuta wakipigana vikumbo kumshangaa Zari ambaye muda mwingi alikuwa akijificha.
Kutokana na mazingira ya watu kukanyagana kutaka kumuona staa huyo, mrembo aliyefahamika kwa jina la Jestina George aligeuka kuwa bodigadi wake ili kumuepushia usumbufu ambapo alifanya kazi ya kumlinda.
PAPARAZI AZUIWA KUMPIGA PICHA
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la msiba kwa lengo la kupata picha za kumbukumbu kwamba Zari aliwahi kufika eneo hilo, alikumbana na wakati mgumu baada ya Jestina kumpiga mkwara asijaribu kupiga picha.
Weee, ukijaribu kupiga picha tunakorofishana, mwenyewe hataki kupiga picha, kama vipi nenda kamuombe ruhusa Diamond, alisema Jestina huku akimficha Zari.....bongonewstz blog