Zawadi bora kabisa ya wakati wote.

Zawadi bora kabisa ya wakati wote.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Niwatakie sikukuu njema mabibi na mabwana.
Tupo wengi tusiokuwa na tabia ya kutoa zawadi,na hata tukitoa hatutoi zawadi bora.
Zawadi ya thamani kabisa,iletayo baraka maishani mwako ni ile to isiyoambatana na masharti ya aina yoyote ile.
Jamani jamani! Usimpe mtoto wa kike hela ili umfunue sketi yake,hata kama ni gari au nyumba haina maana tena.
Usiache kumpa msaada ndugu yako kwasababu tu unajua hawezi/huwa hakusaidii au kukutetemekea! huo nao ni ubatili mtupu.
Usikose kwenda kumzika ndugu wa mfanyakazi mwenzako,eti kwa kuwa nayeye hakuja msibani kwenu.
Mtendee mema asiyeweza kukutendea,mtetee asiyeweza kujitetea,na Mungu atakutetea wewe.
Usimdharau masikini kwa kuwa anayothamani mbele za Mungu wake!!!!Sasa wewe unayemdharau unani labda?
Zaidi kabisa fikiri kabla ya kusema hata kama usemayo ni kweli.
 
Back
Top Bottom