PreGE2025 Zawadi wanazotoa Wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ni Rushwa au la?

PreGE2025 Zawadi wanazotoa Wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ni Rushwa au la?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya Wabunge wanaojitokeza katika majimbo yao na kuanza kutoa misaada mbalimbali, pia kuna Wanasiasa ambao nao sio Wabunge lakini hawakauki kwenye majimbo.

Wengine wanakuwa mbele ya kamera na hadharani kabisa wanatoa zawadi mbalimbali kwa Wananchi au makundi fulani ya Watu kisha kuwaambia hizo ni zawadi au wanawawezesha katika mambo kadhaa

Ninachojiuliza je, hicho kinachofanywa na Wanasiasa kwenye majimbo yao ni Rushwa au ni zawadi kama zilivyo zawadi nyingine za kawaida?

=====================================​

Ikumbukwe, Aprili 30, 2025, akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila aliulizwa swali la aina hiyo na Wanahabari hao

Chalamila alijibu “Kuhusu zawadi, unatakiwa kuangalia je, inatolewa muda gani? Tunaishi wote eneo hili na hujawai kutoa zawadi iweje leo uje utoe zawadi ili hali umetangaza kugombea eneo hili hili, hizo zawadi lazima ziangaliwe.” alisema Chalamila.
 
Back
Top Bottom