JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Usikose kuungana nasi leo Februari 13, 2025, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia XSpaces ya JamiiForums, kwa mjadala wa kina kuhusu zawadi wanazotoa Wanasiasa wakati wa Uchaguzi. Je ni rushwa? Wananchi wanatofautishaje?
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika Mjadala huu, TAKUKURU itafafanua maana ya rushwa katika uchaguzi na vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama rushwa, huku Washiriki wakipata fursa ya kushiriki kwa kutoa maoni, mapendekezo au kuuliza maswali
Kushiriki kupitia XSpaces bofya x.com
William Maduhu:
"Pamoja na Uwepo wa Sheria za kupinga viashiria vya rushwa bado kuna matukio ya wagombea kutoa zawadi kwa Wapigakura"
TAKUKURU hawachukui hatua kushughulikia malalamiko na matukio ya zawadi kutolewa kwa Wapigakura"
Mwaka 2005, LHRC ilitoa changamoto kuhusu suala hilo Kisheria Mahakamani, ndipo Mahakama Kuu ikaeleza kuwa kutoa takrima ni sehemu ya kushawishi Wapigakura, baada ya hapo yakafuata mabadiliko ya Sheria yaliyoondoa vitu vinavyoweza kuchangia ushawishi kwa Wananchi wakati wa Uchaguzi
Pamoja na uwepo wa Sheria kadhaa kupinga viashiria vya rushwa Nchini lakini matukio ya Wagombea au watia nia kuendelea kutoa zawadi kwa Wapigakura bado yapo
Mwaka 2020, TAKUKURU iliwakamata baadhi ya Wagombea kwa kuwa na dalili za kutoa rushwa, baadaye Hayati Rais Magufuli akasema mhusika aliyekamatwa alikuwa na sherehe ya kuzaliwa, hiyo ikachangia TAKUKURU kumuachia mtuhumiwa aliyekamatwaImekuwa ikionekana Wanasiasa wana nguvu ya kupindisha vitu vinavyoashiria suala la Rushwa
Nadhani ni vizuri TAKUKURU wakasema kwanini wanaonekana kutokuwa na Meno makali dhidi ya Wanasiasa au wana hofu kuwa wanapoingia Madarakani wanaweza kuwa mabosi wao"
JOSEPH KASONGWA (TAKUKURU):
"Tunapopokea tuhuma zozote za Rushwa iwe wakati au kabla ya Uchaguzi, inapobainika hivyo suala hilo lazima tulifikishe MahakamaniKuhusu suala la kutangaza Watuhumiwa wa kwanza huwezi kutangaza kila hatua za KimahakamaPia, kuna kulinda Heshima ya Mtu kwa kuwa hizo bado ni tuhuma na tunakuwa katika mchakato wa uchunguzi
Tunasisitiza sana Elimu kwa Wananchi kuwa unapotoa taarifa kuhusu Rushwa basi uwe na wajibu pia wa kutoa ushirikiano zaidi
Sheria ya Rushwa kwa sasa imetuongezea wigo mpana sana, tutafika hadi kwenye Michezo, Bonanza na hata kwenye masuala ya Urembo, Mfano mashindano ya Miss Tanzania"
DKT. ANANILEA NKYA (Mwenyekiti wa Bodi – JUKATA)
"Rushwa haiwezi kuondoka au kupungua kama Mifumo ya kupata Viongozi ndani ya Vyama haitakuwa na mabadiliko, tutakuwa tunaenda mbele na kurudi nyuma na pengine hali kuwa mbaya zaidi
"Watu wengi wanailaumu TAKUKURU, Mimi nasema tusiwalaumu wao kwa kuwa zamani Rushwa ilitolewa waziwazi kwa jina la Takrima tofauti na sasa ambapo inafanyika kwa usiri mkubwaZamani Rushwa ilikuwa inaweza kutolewa kwa njia ya Chakula, Nguo au kitu kingine chochote cha kuwahadaa Wananchi
"Sasa hivi Rushwa inatolewa kwa ukubwa zaidi na kwa kificho kiasi kwamba TAKUKURU ni ngumu kuweza kumkamata Mtu sababu mambo mengi yanafanyika gizani"
ZITTO KABWE (Mwanasiasa ACT Wazalendo):
"Hakuna anayeweza kubisha kuwa kuna matumizi makubwa ya Fedha katika Chaguzi zetu kiasi kwamba ni jambo gumu kutofautisha Rushwa na Zawadi nyakati za Uchaguzi na hasa katika Mwaka wa Uchaguzi
Unaweza kukuta Mgombea ni Rais au Waziri anaweza kutumia nafasi yake wakati wa Kampeni za Uchaguzi kutoa maelekezo ya kimamlaka na hivyo kutumika kama sehemu ya ushawishi wakati ni jambo ambalo halitakiwi kufanyika hivyo
Nilipokuwa nagombea kwa mara ya kwanza Mwaka 2005, nilitumia Tsh. Milioni 13 tu katika Uchaguzi, wakati huo takrima ilikuwa inaruhusiwa na hiyo ilitumika katika mahitaji ya msingi kama Mafuta ya Gari, kukodisha Magari Wenzetu wa CCM ambao walikuwa na nguvu kubwa ya kifedha walitumia nafasi hiyo kutoa Takrima kubwa na kutuumiza wengine.
Kwa sasa sio mjadala tena kuwa kuna Rushwa au hakuna wakati wa Uchaguzi, inajulikana kinachoendelea"
ASSENGA E KIMARO (Mdau)
"Suala sio zawadi, bali kitu kinachotolewa kwa Wananchi wakati au kuelekea katika Uchaguzi kwa asilimia zote hiyo ni Rushwa, sababu Wananchi wao hawatoi ila wanapokea kutoka kwa Wagombea au Watiania
Rushwa ipo, kinachotakiwa TAKUKURU wafanye majukumu yao inavyotakiwa
Tunasema ni zawadi kwa Wananchi, Mgombea anawapongeza nini Wananchi? Hiyo ni rushwa ila tu inatumika katika jina tofauti"
DKT. ANANILEA NKYA (Mwenyekiti wa Bodi – JUKATA)
"Rushwa imetokana na Wananchi kutoamini mifumo ya Uchaguzi, wanaona bora wachukue hela kwa kuwa wanaowachagua wakifika kwenye Uongozi wanaenda kuchukua hela nyingi, hivyo nao wanachukua chao mapema
Sasa hivi Mgombea anaweza kuwa hata na Tsh. Milioni 500 katika Uchaguzi na akakwama kushindaSasa hivi wale waliopo Madarakani na wana nia ya kugombea ndio wanakuwa na hela nyingi na nguvu pia
Tukiendelea hivi tutakuja kujutia kwa kuwa kunaweza kuwa na hatari kubwa zaidi, ninakubaliana na wale wanaosema 'No reform No election'
Tuliona katika Uchaguzi uliopita kuna Kiongozi aliyekuwa Madarakani yeye ndio alikuwa anaamua nani ashindeWagombea wanapitishwa na wenye mamlaka kwa kuangalia “Huyu yupo karibu na mimi” Huyu atanihoji maswali mengi” n.k. Yote hayo yanatokana na kuwepo kwa Mifumo mibovu ya kuchagua Watu"
ZITTO KABWE (Mwanasiasa ACT Wazalendo)
"Jamii ikiamua kudhibiti Rushwa inawezekana, wakati wa Uchaguzi wa Chama kimoja Rushwa ilidhibitiwa sanaBaadaye uchaguzi wa Vyama vingi matumizi ya fedha hayakuwa makubwa lakini kadiri miaka inavyokwenda matumizi ya fedha yanazidi kuongezeka
Rushwa ya Uchaguzi ndio inazaa Rushwa nyingine na kukosekana kwa Uwajibikaji, kwani Kiongozi akishafanya hivyo akashinda lazima atatafuta namna ya kurejesha fedha alizozipoteza awali"
JOSEPH KASONGWA (TAKUKURU)
"Imefika hatua hatuoni kama Rushwa ni adui, hiyo inachangia ugumu wa kupambana nayo, mfano wakati Tanzania ikipambana na Idd Amini, Watanzania wote tulikuwa kitu kimoja, lakini kama wote tukiwa hatuna mtazamo sawa ni vigumu kuizuia Rushwa
Imefika hatua hatuoni kama Rushwa ni adui, hiyo inachangia ugumu wa kupambana nayo, mfano wakati Tanzania ikipambana na Idd Amini, Watanzania wote tulikuwa kitu kimoja, lakini kama wote tukiwa hatuna mtazamo sawa ni vigumu kuizuia Rushwa"
