Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Akichangia Bungeni Kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2025/2026

Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Akichangia Bungeni Kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2025/2026

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. ZAYTUN SWAI, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Akichangia Bungeni Kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2025/2026.

"Katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati mara nyingi tumeona inachelewa kukamilika kwasababu ya kutokuwa na muunganiko mzuri ndani ya Serikali. Wizara zetu za Serikali hazisomani na Taasisi za Umma hazisomani" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kamati ya Bunge ya Bajeti ilikutana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambao walielezea changamoto wanazokutana nazo zinazosababisha kuchelewa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa wakati"

"Mradi wa Liganga na Mchuchuma kama Taifa tumechelewa kunufaika na faida kwasababu ya kuchelewa kutekeleza mradi kwa wakati. Mradi wa Engadi Soda wa Engaruka umeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano na kama ukitekelezwa kwa haraka kama Taifa tutanufaika na faida" - Mhe. Zaytun Seif Swai

"Mradi wa Engadi Soda wa Engaruka utachochea upatikanaji wa Ajira nyingi za Watanzania; Utachochea uanzishwaji wa Viwanda vipya. Malighafi ya Magadi Soda inatumika na Viwanda vya Kemikali, Viwanda vya Kutengeneza Vioo na Mbolea kwenye Kilimo"

Mradi wa Engadi Soda utasaidia kuongeza mapato ya Serikali kupitia Kodi na Tozo mbalimbali. Tutaokoa fedha za kigeni takribani Dola Milioni 120 ambazo kwasasa zinatumika kuagiza Malighafi ya Magadi Soda nje ya nchi"

"Nashauri Serikali itoe kipaumbele kwenye miundombinu yote inayoelekea kwenye miradi ya kimkakati ikiwemo Barabara na Madaraja, Ujenzi wa Malazi Sekta ya Utalii"

"Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Arusha ameleta Miradi mingi ya maendeleo. Kuanzia Mwaka wa Fedha 2021 hadi Septemba 2024 tumepokea zaidi ya Shilingi Trilioni 2.7. Mkoa wa Arusha unachangia takribani Asilimia 4.7 kwenye Pato la Taifa na kuipa nafasi ya Sita kitaifa

Screenshot 2024-11-05 at 11-11-06 TBC Digital (@tbc_online) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-11-05 at 11-11-19 TBC Digital (@tbc_online) • Instagram photos and videos.png
 
Back
Top Bottom