Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Hao jamaa wasipokuwa makini na kuendelea kutumiwa na CCM basi wanaweza kupoteza umaarufu waliokuwa nao. Watanzania wa leo sio wale wa mwaka 47, wanajua kwamba kuna kashfa nzito dhidi ya viongozi wa juu ndani ya sirikali. Hivyo kama watatumiwa ili kubadilisha somo basi watalia kilio cha mbwa maana wananchi wanaweza kabisa kuwageuka wao na kuwaona ni mahayawani tu na umaarufu ukapotea.
 
jamani kwani hao ze comedy hawana akili zao wenyewe za kuona mambo ? Mkuu bubu, mbona wengi wana ile mentality ya kusema kwamba mtu akiwa against na wapinzani basi ametumwa na ccm. after all jamaa ni comedians, kwa hiyo you can expect anything !
 
 
Ukishutumu Ze Comedy umeshutumu dhana potofu waliyokumbatia. Kwa taarifa yako, Ze Comedy sio mtu.

Walioshika glasi yenye sumu ni Watanzania, wakiwemo hao Ze Comedy. Glasi yenyewe ni CCM, na sumu ndani ya glasi ni viongozi wa CCM. Tusipoitupa hiyo glasi, basi sumu yake inaweza ikatatufisha.
 

kwa hiyo unachosema maji safi ni nani ? glasi isiyokuwa na sumu ni nani ? naona upo kwenye kampeni tayari, i dont blame you ! naomba wewe na mwanakijiji mnijibu !
 
Kuna Watanzania milioni 36. Wapo angalau laki moja ambao sio sumu. Wengi wao hawajapata fursa ya kutumikia, kwani "sio wenzetu". Hiyo glasi yenye sumu haina nafasi ya maji safi.

Binafsi, sijawahi kuwa mwanchama wa chama cha siasa. I prefer Maths to Politics. Sasa na milele.
 
Inawezekana kabisa Dr.Slaa ana maovu yake, ila twende mbele turudi nyuma, piga ua galagaza, yote hayo kamwe hayawezi kukanusha madai yake ya ufisadi na orodha aliyoitoa.
 
kwa hiyo fisadi anataja fisadi wenzake ! nashangaa kwa nini hakureserve namba yake mwenyewe huyo Slaa katika hiyo list !
 
Hawa jamaa wakijiingiza kwenye siasa za mafisadi hujue wamekwisha hili ni suala lililo na masirahi kwa taifa siyo la kufanyia mdhaa.

Hivyo ze commedy kutumika katika platform hii haina tofauti9 na TOT ya CCM kwa hiyo usishangae baada ya kuzoea kukandamiza wakajikandamiza wenyewe.

Wamekuwa wakishangiliwa mitaani usione ajabu wakapigwa mawe kuwa ni mafisadi. Mtu yeyote anayemsaidia muhalifu(mbadhirifu) ni hatari kuliko hata mwalifu mwenyewe.
 

Hawa Ze Comedy wameukwaa ukweli mtupu kuhusu huyu jamaa Wilbrod Slaa. I can vouch for the truthfulness of all the above allegations. Bongo siri kwa public personae kama Wanasiasa is hard to come by, and whatever shit they did in the past will one day return to haunt them.
 
Hapa ze comedy kumshambulia slaa ni kuchemsha!

Sisi hatuamuabudu slaa.. ni binadamu kama wengine ana mapungufu yake kama wengine.. hapa cha msingi ni tuhuma alizotoa ni za kweli???

Hapa hata mtumie ze comedy hata mkiwaita kina Fresh prince na Mr Bin wote wamuigize slaa, hata mseme aliua mtu ama alibaka... hageuzwi mtu akili yake na haturudi nyuma ebo!! Yote hayo haya husiani kabisa na kusaini mikataba mibovu na kuchota mabilioni BOT!!

Tumechoka na mafisadi wa CCM kumaliza rasmlai zetu wakijilimbikizia mali na kuacha wengine wote wame duawaa na umasikini ukizidi kujikita!!

Ni aibu kubwa nchi iliyo jaliwa Madini vito kama vile Tanzanite Mito maziwa ardhi yenye rutuba yet eti ni masikini wa kutupwa yaani tunazidiwa na nchi zilizopo jangwani jamani!! Kisa mafisadi wa CCM... Nooooooooo... We are tired of you!

Hapa piga ua galagaza.....Lazima kieleweke!
 
Bora mmesema nyie
 
Hiyo ndio gharama ya kuwa mwanasiasa,si tumekuwa tukikumbushwa hapa JK alipokuwa waziri madini na mamo yote zamani IPTL, NetGroup etc.

Hold on a minute father Slaa, basi hata pesa za vilema?
 
Hold on a minute father Slaa, basi hata pesa za vilema?

Mpaka mungojee wasanii waseme hili.

Mbona mafisadi hawajatamka hili wakati wanajibu hoja zao?

Kwa nini wasiende kwenye mikutano ya Mawaziri wa kuonyesha uzuri wakasema hili?
 
Hoja ya mafisadi itabaki kuwa palepale,siye hatumjui Slaa,hata kama aliua,haituhusu,tunachotaka ni hawa nyang'aus kujibu hoja na kuburuzwa mahakani.Halafu hao Wachekeshaji wenu,wanadai Slaa katembea na mwanamke ndo maana kafukuzwa upadri,hivi kweli mtu na akili yako hii ni hoja kweli,mbona ccm ndo imejaa wabakaji na wahuni wakubwa kabisa.Bwanae hoja kwa hoja,nyie ze comedy hamna lolote lile mkawachekeshe watoto ila watu wazima hawana muda nanyi.
 
Mimi siwajui Ze Comedy and i will be more than happy kama mtu atapost hiyo clip hapa. Ila nimesikia ya kuwa ni maarufu sana huko nyumbani , nadhani hawa watu wamepewa mshiko na CCM ili kujaribu kushift attention ya buzwagi ,Ni kosa kubwa sana kufanya hivyo kwani with time watajishushia hadi waliyojijengea kwa wananchi ! Ni ujinga kujaribu kumsema Dr Slaa kuhusu hizo shutuma mara tuu baada ya kutoa listi ya mafisadi , ninategemea next episode zao watazungumzia kuhusu Rada na Ndege ya rais.
 
Kama Slaa anaona amekashfiwa aende mahakamani....
 
Sasa Serikali inachunguza nini pale BOT? Au na Ze comedy hawajasoma ripoti ya Slaa
Acheni kukuna vichwa na wajinga wale kwani njaa haina adabu, ili wapate kula ni lazima chochote wapewe, sasa kuna hasara gani kwa mafisadi kuwalipa ili kukwepesha mambo hadharani?😕
 

Kada,

Umeliwa! Sisi tunajua mchezo wanaoucheza kina Rostam. Wamewatumia watu wengi kutetea mafisadi kwa njia mbalimbali. Wanalotaka ni kutuondoa kwenye mjadala wa kitaifa ulioibuliwa na wapinzani, laini hatuondoki ng'o! Naona wewe umeshajitumbukiza kwenye viatu vyao, kujaribu kutufanya na sisi tuelekeze mawazo yetu WANAPOTAKA wao. Hivi unafanya makusudi kutimiza haja yao au nawe umekumbwa bila kujua? Bwana ee, turudi square one, tujadili hoja ya msingi. Achana na hoja za kina Rostam na Lowassa kupitia Ze Comedy, tena tutawazomea hata hao Ze Comedy! Kada, amka usingizini usitumiwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…