Hii inanikumbusha mkasa mmoja wa sheha wa shehia moja maarufu kwa kupandikiza wapiga kura kutoka bara kule visiwani, alimkataa mkaazi wake asiandikishwe eti hamtambuwi...ukweli ni kuwa mkaazi huyo alikuwa ni mwanachama wa chama cha upinzani na baraza ya nyumbani kwake ndio kama "masikani" ya mazungumzo na wanachama na wapenzi wa chama chake, siku ya uandikishaji kuelekea uchaguzi wa 2000, jamaa alikataliwa na sheha wake, hakufanya tabu alirudi nyumbani kwake kimya, uchaguzi ukafanyika na yaliyotokea yakatokea. Cha ajabu sasa, zikaja dawa za matende na mabusha, zikawa zinagaiwa kila nyumba katika kila shehia na masheha wakatakiwa wawahamasishe wakaazi wa shehia zao kuchukuwa dawa hizo, sheha yule yule, kiguu na njia katika vijumba vya wakaazi wake, akiwataka kushirikiana na watoa dawa...alipofika katika nyumba ya yule jamaa aliyemnyima kuandikishwa siku ya uchaguzi... kwa mbwembwe za ukubwa wa kuongoza mtaa tu..alianza upuuzi wake...si anajuwa kuwa jamaa ni mpinzani "...hodi.." aliita bw.sheha kwa kelele. Bahati jamaa alikuwapo, mlango ulipofunguliwa tu,sheha hakusubiri, alitoa ilani kwanza. "...nimekuja makusudi kwa habari za dawa za matende maana nasikia mnakataza watu wasichukuwe eti zinaharibu uzazi..uwongo mtupu..." alin'gaka sheha. Kwani aliwahi kumaliza, mke wa yule jamaa kama alipangwa vile alivurumisha dishi la maji ya mavumba,yananuka vibaya sijuwi yalivumbikwa siku ngapi, na jamaa baada ya kumtaka radhi sheha, aliporomosha matusi na kumfukuza "..nenda kashitaki popote ww si mkubwa, alaaa...kwenye kura hunitambuwi...kwenye madawa haya hata sijuwi yanatoka wapi...huko unanitambua...mm sina haja ya dawa bana...pelekeni hospitali huko...hata panadolo hakuna..eboo..." alimalizia kwa msonyo na kufunga mlango wake. Mbona uchaguzi uliofuata aliandikishwa.