Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imemuengua Bw.Hamad Masoud Hamad kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha wananchi- CUF kwa kutokukidhi kigezo cha kuwa wanachama mia mbili katika mkoa wa Kaskazini Unguja huku mgombea wa ACT wazalendo Bw.Othman Masoud Othman akitakiwa mpaka kesho saa tatu asubuhi awe amewasilisha katika tume hiyo majina ya wanachama wake wa mikoa ya Kaskazini Unguja na Kusini Unguja.