PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetoa rasmi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2025, ikieleza kuwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa CCM alishinda urais kwa kupata kura 448,892 (74.79%), huku Othman Masoud Othman wa ACT-Wazalendo akipata kura 139,399 (23.22%).
Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa uchaguzi uligharimu Shilingi bilioni 12.26 zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku changamoto zilizobainishwa zikijumuisha taarifa za upotoshaji, maandalizi ya mawakala wa vyama na matatizo ya mtandao katika malipo ya watendaji wa muda, pamoja na mapendekezo ya kuboresha taratibu za uchaguzi ujao.
Soma >> Uchaguzi wa Urais Zanzibar: Dkt. Hussein Mwinyi ashinda kwa 74.80%
Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Mwaka 2025 iliyotolewa rasmi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mwaka 2026:
Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa uchaguzi uligharimu Shilingi bilioni 12.26 zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku changamoto zilizobainishwa zikijumuisha taarifa za upotoshaji, maandalizi ya mawakala wa vyama na matatizo ya mtandao katika malipo ya watendaji wa muda, pamoja na mapendekezo ya kuboresha taratibu za uchaguzi ujao.
Soma >> Uchaguzi wa Urais Zanzibar: Dkt. Hussein Mwinyi ashinda kwa 74.80%
Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Mwaka 2025 iliyotolewa rasmi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mwaka 2026:
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Zanzibar
- Mshindi wa Kiti cha Urais: Dkt. Hussein Ali Mwinyi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) alitangazwa rasmi kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura 448,892 (74.79%).
- Mshindi wa Pili: Othman Masoud Othman kutoka Chama cha ACT-Wazalendo alipata kura 139,399 (23.22%).
- Ushiriki wa Wapiga Kura: Jumla ya wananchi 609,096 (84.88%) walijitokeza kupiga kura kati ya wapiga kura 717,557 waliosajiliwa.
Matokeo ya Baraza la Wawakilishi na Viti Maalumu
- Viti vya Kuchaguliwa (Majimbo 50):
- CCM: Ilipata ushindi katika majimbo 40.
- ACT-Wazalendo: Ilipata ushindi katika majimbo 10.
- Uteuzi wa Viti Maalumu vya Wanawake (Viti 20):
- CCM: Ilipata viti 16 (sawa na 80% ya uwiano).
- ACT-Wazalendo: Ilipata viti 4 (sawa na 20% ya uwiano).
Matumizi ya Fedha na Bajeti ya Uchaguzi
- Uchaguzi huo ulikadiriwa na kutumia Tsh. 12,260,588,000/= ambapo 100% ya fedha hizo ziligharamiwa na Mfuko Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) bila kutegemea ufadhili wa nje.
- Ukaguzi wa ndani ulithibitisha matumizi yote ya fedha yalizingatia Sheria na Kanuni za Usimamizi wa Fedha za Umma.
Mambo Mapya na Uvumbuzi Kwenye Uchaguzi wa 2025
- Kura ya Mapema (Early Voting): Ilifanyika Oktoba 28, 2025 ambapo jumla ya wapiga kura 60,844 waliwasilisha maombi na kupiga kura katika maeneo 50 yaliyoidhinishwa.
- Kifaa cha Nukta Nundu (Tactile Ballot Folder): Kilitumika kuwawezesha Watu Wenye Ulemavu wa uoni kupiga kura kwa siri bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine.
- Mfumo wa Kidijitali wa Waangalizi (OMS): ZEC ilizindua Mfumo wa Observers Management System uliosaidia kusajili na kutoa vibali kwa waangalizi wa ndani na wa kimataifa kwa njia ya mtandao.
Hali baada ya Uchaguzi na Mashauri ya Kisheria
- Wagombea kutoka chama cha ACT-Wazalendo walifungua mashauri ya uchaguzi katika majimbo 25 na wadi 1 wakilalamikia ukiukwaji wa taratibu.
- Baada ya pingamizi za awali kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu, Mahakama Kuu iliyatupilia mbali/kuyafuta mashauri hayo kwa mapungufu ya kisheria.
Mafanikio, Changamoto na Mapendekezo
- Mafanikio: Serikali kugharamia uchaguzi kwa 100%, amani na utulivu kutawala, kiwango cha juu cha ushiriki wa wapiga kura (84.88%), utumiaji wa majalada ya nukta nundu (tactile ballot folder) kwa walemavu wa uoni, na kutangazwa kwa matokeo ndani ya muda wa kisheria.
- Changamoto: Baadhi ya vyama kutosomesha mawakala wao, nafasi finyu vituoni kutokana na idadi ya mawakala wa ZEC na INEC, changamoto za mtandao wa simu katika kulipa watendaji wa muda, na taarifa za upotoshaji.
- Mapendekezo: Kufanya marekebisho ya sheria ili kupunguza idadi ya mawakala vituoni, kuanzisha huduma ya kwanza (first aid) vituoni, na kuweka mifumo bora zaidi ya malipo ya watendaji wa muda badala ya mifumo ya mtandao wa simu.