Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewasiri nchini uturuki kwa ajili ya mazungumzo ya usitishwaji wa mapigano huko Ukraine ambako inatazamiwa kuwa majadiliano yanahudhuliwa na Recep Erdogan
Kando na hayo Rais wa urusi voldmil putin yeye ametumiwa wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo hayon na raisi wa Ukraine huku Vladimir Medinsky akiongoza kikosi cha urusi kwenye mazungumzo
Zelenskyy amesema kuwa ujumbe wa Ukraine unajumuisha waziri wake wa mambo ya nje, wakuu wa jeshi na ujasusi na pia maafisa wakuu kutoka ofisi yake
Katika hatua nyingine Rais wa urusi Vladmir putin , ambaye mwenyewe amependekeza mazungumzo hayo amekataa mwaliko wa Zelensky wa kufanya mkutano wa ana kwa ana
Kabla ya mazungumzo kufanyika Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kwamba wanajeshi wa Urusi wameteka vijiji vingine viwili katika eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine huku Moscow imeendelea na uvamizi wake kamili wa maeneo Jirani
Raisi wa Ukraine amezungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kuwasili mjinji Ankara amesema kuwa hatua zinazofuata za mazungumzo zitaamuliwa baada ya mkutano wake ujao na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Kwa sasa mazungumzo ya kutafuta usitishwaji wa mapigano huko unaongonzwa na Vladimir Medinsky, msaidizi wa Putin ambaye ataongoza kikosi cha urusi kikiwa na maafisa watatu wa ngazi za juu
Kauli ambayo imetolewa na Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakushangaa kwamba Putin ameshindwa kuhudhulia mkutano huo ikumbukwe Trump amekuwa akishinikiza Putin na Zelenskyy kukutana kwa ajilin yab mazungumzo
Maelezo kuhusu ikiwa, lini na wapi ujumbe wa Ukraine unaweza kukutana na wenzao wa Urusi bado haufahamiki lakini yanatarajiwa kufafanuliwa baada ya Zelenskyy na Erdogan kukutana.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema kwamba Washington "haikuwa na Subira na iko tiari kuzingatia utaratibu wowote ili kufikia makubaliano ya vita
Amenukuliwa akizungmza katika mkutano huko Antalya Ni wazi, tuko katika hali ngumu sana hivi sasa, na tunatumai kuwa tunaweza kupata hatua mbele ambazo zinatoa mwisho wa vita hivi kwa njia ya mazungumzo na kuzuia vita vyovyote katika siku zijazo," Rubio alisema katika mkutano wa Nato huko Antalya.