Zelensky anaposifia silaha za Marekani hana nia nzuri na dunia

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kila siku raisi wa Ukraine anapotaka kujisifu kuwa amekomboa eneo au tuseme anapopiga propaganda za vita hawachi kusifu silaha fulani aliyopokea karibuni kutoka Marekani au kwa washirika wake.

Na anaponyimwa chochote na nchi hizo hawachi kutoa lawama za wazi wazi na vitisho kwa taifa hilo kwa kumnyima alichotaka.

Kwa ukweli tabia hizi ni za kupimwa sana na watu wanaotoa ushirikiano naye,kwani inaonesha wazi kuwa nia yake ni kugombanisha mataifa ili dunia iingie kwenye vita ya tatu ya dunia.Sijui kwa hili anatamani apate nishani ya aina gani na inashangaza kwamba mataifa makubwa yanakokotwa kuelekea kwenye balaa mithili ya chatu anavyomla mbwa.
 
Mkuu subiri kwanza aendelee kumtoa adui nyumbani mwake, hizo silaha ni za kusifiwa kwakweli mana Russia alivamia na msururu wa vifaru vya USSR kutoka mbagala hadi posta kumbe wenzake wana kitu kidogo tu unaeka begani unapiga kilomita zote hizo.,
 
... Kiongozi ule msafara uliripotiwa kufikia 64km; umbali sawa na Dar City Centre to Ruvu Darajani mbele ya Mlandizi. Sasa kuulinganisha na Mbagala - Posta pasipofikia hata 20km unakosea.

Ila Javelin ipewe heshima jinsi ilivyoupoteza kama umande wa asubuhi na kwa hakika kwa kizazi hiki hapatatokea tena msafara wa kijeshi wa kipumbavu namna ile.
 
Russia anatumia elimu ya vita ya pili ya dunia kupigana miaka hii
 
Mkuu subiri kwanza aendelee kumtoa adui nyumbani mwake, hizo silaha ni za kusifiwa kwakweli mana Russia alivamia na msururu wa vifaru vya USSR kutoka mbagala hadi posta kumbe wenzake wana kitu kidogo tu unaeka begani unapiga kilomita zote hizo.,
Mbagala mpaka Posta ni karibu.Na hili ni kosa kubwa la kivita alilofanya Putin.Hakujifunza yaliyompata Afghanistan miaka ile.Pamoja na hivyo tujue silaha za nyuklia anazo na akiamua kuzitumia sote tutatimua mbio.
 
... Kiongozi ule msafara uliripotiwa kufikia 64km; umbali sawa na Dar City Centre to Ruvu Darajani mbele ya Mlandizi. Sasa kuulinganisha na Mbagala - Posta pasipofikia hata 20km unakosea.

Ila Javelin ipewe heshima jinsi ilivyoupoteza kama umande wa asubuhi na kwa hakika kwa kizazi hiki hapatatokea tena msafara wa kijeshi wa kipumbavu namna ile.
Alifanya kama hivyo alipoingia Crimea na hakupata hasara yoyote.Safari hii hakujua adui alikuwa ameota mapembe.Askari wake walioangamia kwenye msafara ule ndio imekuwa ujumbe wa woga kwa jeshi zima lililobakia.
 
Kila siku raisi wa Ukraine anapotaka kujisifu kuwa amekomboa eneo au tuseme anapopiga propaganda za vita hawachi kusifu silaha fulani aliyopokea karibuni kutoka Marekani au kwa washirika wake.

Na anaponyimwa chochote na nchi hizo hawachi kutoa lawama za wazi wazi na vitisho kwa taifa hilo kwa kumnyima alichotaka.

Kwa ukweli tabia hizi ni za kupimwa sana na watu wanaotoa ushirikiano naye,kwani inaonesha wazi kuwa nia yake ni kugombanisha mataifa ili dunia iingie kwenye vita ya tatu ya dunia.Sijui kwa hili anatamani apate nishani ya aina gani na inashangaza kwamba mataifa makubwa yanakokotwa kuelekea kwenye balaa mithili ya chatu anavyomla mbwa.
Zelensky namfananisha na Arturo Romanio wa money Heist
 
Alifanya kama hivyo alipoingia Crimea na hakupata hasara yoyote.Safari hii hakujua adui alikuwa ameota mapembe.Askari wake walioangamia kwenye msafara ule ndio imekuwa ujumbe wa woga kwa jeshi zima lililobakia.
... intelligence yake ilikwama wapi isimshauri kwamba zama zimebadilika? Au ni kiburi tu cha usupa pawa?
 
Mbagala mpaka Posta ni karibu.Na hili ni kosa kubwa la kivita alilofanya Putin.Hakujifunza yaliyompata Afghanistan miaka ile.Pamoja na hivyo tujue silaha za nyuklia anazo na akiamua kuzitumia sote tutatimua mbio.
Mkuu tuliza mpira silaha za nuclear zinaongozwa na mfumo maalum (system), west wako macho 24hrs kuweza ku-interupt, putin ni mtoto mchanga sana vita ni plans na strategies, US wako makini sana
 
West wameanza kuokota Kuni mwituni wako makini?
USA na skendo ya uchaguzi wapo makini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masheikh humu wanapiga domo tu hawajui hata hiyo nyuklia anaanzishwaje wanafikiri inarushwa tu kama anayerusha mkuki mnadani Kibaigwa.

They know nothing concerning Nuclear Armament Launch Principle which provides no clandestine approach prior to the launch thus making the whole strategy known before hand.
 
Blah blah blah za pro putin kwisha humu, sisi wenyewe tuna ya kwetu wewe kutwa JF kushabikia Russia ambao ndio wavamizi, na bado watapigwa sana winter hiyoooo inasogea, sasa vita itabaki Ile ya man to man,conventional war russia chini
 
Kwani HIMARS imekomboa vijiji vingapi?
hili swali tushalijibu.
Pro russia chukueni mic[emoji441] Swali lingine Tafadhali.
 
... Kiongozi ule msafara uliripotiwa kufikia 64km; umbali sawa na Dar City Centre to Ruvu Darajani mbele ya Mlandizi. Sasa kuulinganisha na Mbagala - Posta pasipofikia hata 20km unakosea.

Ila Javelin ipewe heshima jinsi ilivyoupoteza kama umande wa asubuhi na kwa hakika kwa kizazi hiki hapatatokea tena msafara wa kijeshi wa kipumbavu namna ile.
Soviet era tactics
 
Back
Top Bottom