Zelensky kwanini NATO na sio EU?

Zelensky kwanini NATO na sio EU?

Kitu hiki kinanishangaza sana na kuona kua kumbe Kuna baadhi ya Viongozi wazungu ni wajinga sana.

Zelensky wa Ukraine ameng'ang'ania kutaka kujiunga na umoja wa kujihami kijeshi wa nchi za Magharibi ambao hauna faida yoyote ya kiuchumi na kisiasa zaidi ya ulinzi wa kijeshi.

Nashangaa kwa sababu Kuna nchi nyingi zilizokua umoja wa Soviet wala hazina haja na NATO na maisha yanaendelea vizuri TU,mfano Tajikistan,kyugistan, Georgia,Azebaijan,Beralus n.k

Ni kweli ukiangalia hakika NATO Haina msaada kiuchumi Bali kijeshi,je kwa Nini zelensky na Ukraine wanatamani sana kujiunga na NATO badala ya kutamani kujiunga na umoja wa Ulaya (European Union)?ambao kwa hakika unafaisa sana kiuchumi badala ya kijeshi?

Je zelensky na Ukraine Wana nia gani na Wana malengo gani ya
kivita na kijeshi?

Kabla ya hii vita na kabla ya mapinduzi ya Maidan na wakati wa Marais wa Ukraine wa kabla ya ya Zelensky akina Leonid kravchuk,Leonid kuchma ,Petro Poroshenko,na Victot Yanukovic kulikua Kuna amani na mahusiano mazuri baina ya Urusi na Ukraine.

Swali langu ni Kwa Nini Ukraine ya Sasa hawana shida na kujiunga na miungano ya kiuchumi na kisiasa kama Shanghai cooperation,G20 na EU,bali wanatamani kujiunga Kwa jasho na damu na umoja wa kijeshi na kivita wa NATO kwa Kila namna?

Hii ni akili ya namna Gani?

Kwa Nini NATO isiyo na faida kiuchumi? na kibaya zaidi inakugombanisha na jirani Yako?
Hii ni akili ya namna Gani?

Zelensky na Ukraine ya Sasa wamekusudia Nini na wana malengo Gani?na NATO
Kwani Kuna ulazima Gani na NATO badala na EU?
Tatizo lilianzia kwenye uchaguzi ule ambao ulimtoa Yanukovich madarakani na kupelekea Maidan Revolution .
Ukiwa kiongozi lazima ujue watu wanataka nini, na si kwa matakwa ya kiongozi.
Ndio maana ya uchaguzi, Zelensky asipowapa wanachokitaka - watamnyongelea Mbali- as simple as that .
 
Umetaja nchi ambazo zilikua umoja wa Soviet na hazina haja na NATO, kwenye list yako umesahau UKRAINE kwa sababu ni nchi yenye maendeleo makubwa sana kiuchumi na kijeshi na inarasilimali nyingi sana ambazo zinaweza kuifanya ikawa tajiri na kuitishia Russia kama itaungana na adui wa Russia...Ukraine haina shida ya uchumi kama unavyodhani, inashida ya ulinzi kwa sababu Russia haitaweza kukubali kuziacha rasilimali za Ukraine
Rasimali gani ambazo Ukraine anazo ila Urusi hana?
 
Zelensky wa Ukraine ameng'ang'ania kutaka kujiunga na umoja wa kujihami kijeshi wa nchi za Magharibi ambao hauna faida yoyote ya kiuchumi na kisiasa zaidi ya ulinzi wa kijeshi.
Faida ya kiusalama ni muhimu katika uchumi, ni nchi gani kubwa kiuchumi ambayo haina jeshi kubwa?

Ukisema NATO haina faida ni kwamba huijui, tangu ianzishwe hakuna nchi mwanachama aliwahi vamiwa na NATO imefanikiwa kuzuia nchi wanachama kupigana.
Nashangaa kwa sababu Kuna nchi nyingi zilizokua umoja wa Soviet wala hazina haja na NATO na maisha yanaendelea vizuri TU,mfano
Hizo nchi haziishi kwa kuangaliziana, hazilazimiki kufanana wala kuigana. Kila nchi na matakwa yake na isipangiwe muungano.
Tajikistan
Haijawahi tishiwa kuvamiwa na Urusi.
kyugistan
Kyrgyzstan haijawahi tishiwa kuvamiwa na Urusi.
Ilivamiwa na Urusi sababu haikuwa NATO. Ikagawanywa Southern Ossetia na Abkhazia.
Azebaijan
Haijawahi tishiwa kuvamiwa na Urusi. Ila Urusi iliiunga mkono Armenia kwenye mgogoro wa Nagorno Karabakh. Azerbaijan ikawa na support ya Israel na Turkey, wakashinda influence ya Urusi. Urusi asingevamia akashindane tena na Uturuki maana huwa inamuumbua refer Libya na Syria.
Haijatishiwa kuvamiwa na Urusi na inapewa misaada ya kijeshi. Wala EU au NATO hawajaing'ang'ania kama ambavyo Urusi inajilazimisha kwa Ukraine.
Ni kweli ukiangalia hakika NATO Haina msaada kiuchumi Bali kijeshi,je kwa Nini zelensky na Ukraine wanatamani sana kujiunga na NATO badala ya kutamani kujiunga na umoja wa Ulaya (European Union)?ambao kwa hakika unafaisa sana kiuchumi badala ya kijeshi?
Kwanini Urusi isijiunge European Union, kwani haitaki kukua kiuchumi?

Ukraine iliomba kujiunga EU na wanapitia ombi hilo pamoja na ombi la Moldova. Nani walikueleza Ukraine haitaki EU, sijui ni Warusi.

Unajua chanzo cha Maiden Revolution ya 2013 hapo Ukraine?
Je zelensky na Ukraine Wana nia gani na Wana malengo gani ya
kivita na kijeshi?
Kulinda nchi yao. Thats all.
Kabla ya hii vita na kabla ya mapinduzi ya Maidan na wakati wa Marais wa Ukraine wa kabla ya ya Zelensky akina Leonid kravchuk,Leonid kuchma ,Petro Poroshenko,na Victot Yanukovic kulikua Kuna amani na mahusiano mazuri baina ya Urusi na Ukraine.
Kabla ya Zelensky, Urusi haikuvamia Ukraine. Urusi ilivamia February 2022 ambapo Rais alikuwa Zelensky.

Kabla ya Zelensky, Urusi iliiteka Crimea na kuitwaa. Baada ya hapo mahusiano yakafa kabla hata Zelensky hajaja.
Swali langu ni Kwa Nini Ukraine ya Sasa hawana shida na kujiunga na miungano ya kiuchumi na kisiasa kama Shanghai cooperation,G20 na EU,bali wanatamani kujiunga Kwa jasho na damu na umoja wa kijeshi na kivita wa NATO kwa Kila namna?

Hii ni akili ya namna Gani?
Ukraine wanaitaka EU.

Kwanini Urusi isiivamie NATO, iende kuivamia Ukraine ambaye ni jirani. Hii ni akili ya namna gani?

Ukraine kwa jasho na damu inaitaka NATO sababu Urusi hajawahi peleka pua yake kwenye muungano huo.
Kwa Nini NATO isiyo na faida kiuchumi? na kibaya zaidi inakugombanisha na jirani Yako?
Hii ni akili ya namna Gani?
Kwani Ukraine hajui kuwa NATO sio ya kiuchumi. Ukraine inajua mahitaji yake kuliko wewe ambaye hata sio raia.
Zelensky na Ukraine ya Sasa wamekusudia Nini na wana malengo Gani?na NATO
Kwani Kuna ulazima Gani na NATO badala na EU?
Zelenksy na Ukraine wanataka kujiunga EU na NATO, vyote. Huo ulazima usiouona wao wanauona na huna mamlaka ya kuwapangia wasiuone, hata Urusi haina mamlaka hayo.

Mwisho, Urusi ilivamia Ukraine 2014. Ikavamia tena February 2022. Ukraine ikaomba kujiunga NATO mwezi September 2022.

Urusi iliivamia Ukraine kwanza 2014 Crimea, ikapigana vita Mashariki mwa Ukraine, ikadungua ndege ya abiria, ikaua maelfu na kuwahamisha makazi. Kisha ikavamia tena 2022 vita mpaka leo.
Meanwhile, Poland na Finland majirani wa Urusi wapo NATO na hawajahi vamiwa na Ukraine. Turkey inapigana na maslahi ya Urusi na kudungua ndege zake ila haijawahi vamiwa sababu ipo NATO. Akili za mtoto zitakwambia kwanini Ukraine inaitaka NATO.

Na kwa kukujulisha tu, Ukraine kwa sasa kipaumbele ni usalama sio uchumi. Siwezi kuja kwako na panga kukuumiza, wewe badala ushike silaha kupambana ndio kwanza unashika fuko la fedha ukalifiche uvunguni. Sasa si nitakuua nilichukue. Yani Tanzania tumevamiwa vita ya Kagera 1978 wewe unakomaa na Vijiji vya Ujamaa na Azimio la Arusha.
 
Rasimali gani ambazo Ukraine anazo ila Urusi hana?
Watanzania tunaakili kwamba kama leo tuna unga na dagaa ndani ya kesho yatajisumbukia, wenzetu wanapanga miaka 200 mbele na hapo ndo wametuzidi. Ukijua kuwa Marekani ina mafuta mengi ya kuchimba karne na karne ila hawagusi wanapambana na mafuta ya watu utajua mzungu haangalii leo...
 
Kitu hiki kinanishangaza sana na kuona kua kumbe Kuna baadhi ya Viongozi wazungu ni wajinga sana.

Zelensky wa Ukraine ameng'ang'ania kutaka kujiunga na umoja wa kujihami kijeshi wa nchi za Magharibi ambao hauna faida yoyote ya kiuchumi na kisiasa zaidi ya ulinzi wa kijeshi.

Nashangaa kwa sababu Kuna nchi nyingi zilizokua umoja wa Soviet wala hazina haja na NATO na maisha yanaendelea vizuri TU,mfano Tajikistan,kyugistan, Georgia,Azebaijan,Beralus n.k

Ni kweli ukiangalia hakika NATO Haina msaada kiuchumi Bali kijeshi,je kwa Nini zelensky na Ukraine wanatamani sana kujiunga na NATO badala ya kutamani kujiunga na umoja wa Ulaya (European Union)?ambao kwa hakika unafaisa sana kiuchumi badala ya kijeshi?

Je zelensky na Ukraine Wana nia gani na Wana malengo gani ya
kivita na kijeshi?

Kabla ya hii vita na kabla ya mapinduzi ya Maidan na wakati wa Marais wa Ukraine wa kabla ya ya Zelensky akina Leonid kravchuk,Leonid kuchma ,Petro Poroshenko,na Victot Yanukovic kulikua Kuna amani na mahusiano mazuri baina ya Urusi na Ukraine.

Swali langu ni Kwa Nini Ukraine ya Sasa hawana shida na kujiunga na miungano ya kiuchumi na kisiasa kama Shanghai cooperation,G20 na EU,bali wanatamani kujiunga Kwa jasho na damu na umoja wa kijeshi na kivita wa NATO kwa Kila namna?

Hii ni akili ya namna Gani?

Kwa Nini NATO isiyo na faida kiuchumi? na kibaya zaidi inakugombanisha na jirani Yako?
Hii ni akili ya namna Gani?

Zelensky na Ukraine ya Sasa wamekusudia Nini na wana malengo Gani?na NATO
Kwani Kuna ulazima Gani na NATO badala na EU?
Trump alimpasha huyu shoga zelenskyy kuwa anachezea Shilingi kwenye tundu la choo kwamba world war three inaweza tokea halafu li Zelenskyy linabana pua tu hahahaha, ninavyoons he will be disposed
 
Naomba unielezee maana yake ,jukwaa hili tunapeana Elimu na maarifa.
A 'Sovereign State' is defined as a political entity that holds the right to domestic autonomy and the ability to enter into treaties independently with other entities, excluding external sources of authority both in theory and in practice."
 
Je Mexico,na Cuba hazina hadhi au Hali hiyo?
Kwa mfano mexico na Cuba zikaomba kupewa ulinzi wa kijeshi toka Urusi zitakubaliwa?
 
Trump alimpasha huyu shoga zelenskyy kuwa anachezea Shilingi kwenye tundu la choo kwamba world war three inaweza tokea halafu li Zelenskyy linabana pua tu hahahaha, ninavyoons he will be disposed
Uko sahihi kabisa Mkuu.
Na zelensky alikua anachagiza sana USA na NATO waingie rasmi vitani,bila kujua madhara yake.
Trump amemgundua jamaa ni kiparumba mno.
 
Umetaja nchi ambazo zilikua umoja wa Soviet na hazina haja na NATO, kwenye list yako umesahau UKRAINE kwa sababu ni nchi yenye maendeleo makubwa sana kiuchumi na kijeshi na inarasilimali nyingi sana ambazo zinaweza kuifanya ikawa tajiri na kuitishia Russia kama itaungana na adui wa Russia...Ukraine haina shida ya uchumi kama unavyodhani, inashida ya ulinzi kwa sababu Russia haitaweza kukubali kuziacha rasilimali za Ukraine
Ukraine hii ya akina pro west ndio yenye tabu ila ya post soviet na wale pro russia leaders ilokuwa iko poa sana tu kwa russia ila hii ya kuleta adui kwenye boda ya russia wacha ifumuliwe na ivunjwe vunjwe lazima russia ijiwekee buffer zone
 
Uko sahihi kabisa Mkuu.
Na zelensky alikua anachagiza sana USA na NATO waingie rasmi vitani,bila kujua madhara yake.
Trump amemgundua jamaa ni kiparumba mno.
Sana ni jamaa jinga mno. Unajua wa Ukraine wengi ni kama wapemba wa bongo, hivi leo ukisema bara na visiwani tuuane na afaidike oman au Iran hivi ni akili???
 
Nili mnukuu trump akisema ndani ya two weeks. Angemaliza hiyo vita. Cha kushangaza zele hakusema kitu.

Kulikua hakuna haja ya hiyo vita ikiwa TU. Wisdom ingetumika.
 
Ukraine hii ya akina pro west ndio yenye tabu ila ya post soviet na wale pro russia leaders ilokuwa iko poa sana tu kwa russia ila hii ya kuleta adui kwenye boda ya russia wacha ifumuliwe na ivunjwe vunjwe lazima russia ijiwekee buffer zone
Ningekua Putin ningefanya hvyo Ningekua Zalensky ningefanya hvyo pia
 
Back
Top Bottom