Ernesto Che
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,114
- 293
Habari wakuu,
Nimekuwa msikilizaji mzuri wa kipindi cha supa mix cha East africa Radio kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana. Kipindi hiki kinatangazwa na Zembwela (mchekeshaji wa zamani) na mwanadada mwingine.
kinachonikera katika kipindi hiki ni upotoshaji mkubwa wa Zembwela, ambaye siamni kama ana elimu nzuri (kulingana na hoja zake) zaidi ya kuongea mambo asiyoyajua hovyo hovyo. Kazi yake kubwa ni kukebehi wabunge, serikali za mitaa n.k. bila kutoa uchambuzi yakinifu. Utangazaji huu haufai kwa maendeleo ya taifa kwani mtangazaji anatakiwa kuchambua jambo ambalo ana ufahamu nalo, na iwapo hana ufahamu wa kutosha basi aalike wataalamu wa fani husika ili watoe habari kwa kina.
Zembwela anaropoka ovyo kiasi cha kukera wasikilizaji makini,
Rai - Zembwela ulikuwa mchekeshaji mahiri, usikurupukie fani ambazo una uelewa finyu. Nakushauri uwe na busara ukufahamu kuwa unasikiliza na watanzania wenye uelewa tofauti, punguza uropokaji usio na tija.