Zembwela na Mpoki, nani unamkubali?

Zembwela na Mpoki, nani unamkubali?

Pengine hawa watu ni vigumu kuwalinganisha sana kwa kuwa naona hawana ufanania kwa sana!

Bila shaka kila mtu kabobea kwa upande wake
Mpoki amebobea kwenye vichekesho na ana uwezo wa hali ya juu! Lakini ukimleta upande mwingine hasa ukimwambie asichekeshe uwezi kumuona kama ni yeye!

Kwa upande wa Zembwela naye ni mchekeshaji lakini si kiwango cha mpoki ..uzuri wa Zembwela anaweza kuwa MC katika mazingira yote hata kama hakuhitajiki vichekesho!

Zembwela ni mmoja wa watangazaji ambao wamebarikiwa uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na kuhoji mwanzo ..uwezo wake ni mzuri sana kuliko watu wengi tunao wajua wamesoma!

Kwao hiyo naweza sema Zembwela ana vipaji vingi sana na anajua jinsi ya kuvitumia!

Kiufupi Mpoki na Zembwela kila mtu anaweza sehemu aliyopo na ana itendea haki!

babu mkombe wa kulichombe, mpenda pombe kwa kikombe mbele ya wapambe, ukimkuta bar usimuombe pombe, msubir nyumban akupe eembee... anakwambia UKO SAWA KABISA WEWE
 
Back
Top Bottom