Hahahaaa hapana haijatangazwa popote wanajamvi Bali ni Mimi mwenyewe nimeamua kuwaza kwa sauti!
Sio siri huyu Zembela nimejaribu kumfatilia kwenye kipindi cha super mix East African Radio pia kipindi cha uswazi pale EATV nimegundua jamaa anaupeo mkubwa wa kupambanua mambo pia ni jamaa aliekulia kitaa hivyo jiji la Dar es salaam analijua nje ndan na shida za watu wake!
Pliz nisieleweke tofauti labda nampigia debe Zembela la hasha nawaza tu,laiti ingekua mm mkulu ningempa jamaa ukuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Karibuni wanajamvi tufikiri pamoja kwa sauti...
Ni wazo zuri tu, tatizo umelikuza/umelipanua sana...!!
Kwa nini hukufikiria apewe angalau Ukuu wa wilaya tu, tena wa Temeke..
Huku ndiko angalau kwa Elimu na huko unako msemea kuwa ana Upeo na uzoefu wa maisha ya Wana dalisalaam (waswahili walio wengi) angeweza kutendea haki mshahara atakao lipwa..
Sifa kubwa ambayo angekuwa nayo Mkuu wa Mkoa wa Dar (nawaza tu) angekuwa na Elimu ya juu ya Engineering, MUHANDISI wa Mipango Mji/Mwenye uwezo mkubwa wa kukaa na Kubuni,Kuchora na kuelekeza...
Tatizo linalo ukabili Mji/Jiji la Dar, ni Miundombinu, ujenzi holela (wa hovyo hovyo) na Uchafu uliokithiri....
Sifa ya kuondoa umasikini kwa Raia, sio kipaumbele katika Mji wenye mipango na Mazingira (miundombinu) bora kwa wananchi wake...
Umasikini ungalipo katika miji yote mikubwa duniani.
Sio Nairobi, Rio de Jeneiro, Capetown, London, Brussels na mingine mingi...
Sent using
Jamii Forums mobile app