HAPA WATANZANIA NDIO TUNAPOFELI. YANGA WAMEFANYA UZEMBE MKUBWA SANA HALAFU MNAKUJA HUKU MITANDAONI KUSIFIA UJINGA, MATOKEO YAKE WACHEZAJI WAKIONA HIVI WANABWETEKA IKIFIKA MECHI YA MARUDIANO TIMU INAFUNGWA INARUDI KICHWA CHINI.
KWA KWELI NAWALAUMU SANA WACHEZAJI WA YANGA BADALA YA KUTUMIA FAIDA YA UWANJA WA NYUMBANI WAO WAKALEWA SIFA KWA KAGOLI KAMOJA WAKARUDI WAKAPAKI BASI. IWAPO YANGA WANGEKUWA MAKINI ILE MECHI ILIKUWA INAISHIA HAPA DAR KWANI WALIKOSA GOLI TATU ZA WAZI PAMOJA NA KUPAKI BASI. IWAPO WANGETAMBUA FAIDA YA UWANJA WA NYUMBANI WAKAFUNGUKA KWA KWELI ZESCO ANGEFUNGWA GOLI ZAIDI YA MBILI.
VIONGOZI NA MAKOCHA WANAPASWA WAWAPE SEMINA WACHEZAJI NA HASA YULE KIPA MNATA KUWA CHAMPIONS LEAGUE SIO SAWA NA LIGI KUU BARA. TIMU PINZANI IKIJA KWAKO WAKIJICHANGANYA PIGA GOLI ZA KUTOSHA KWANI KUSHINDA UGENINI KWENYE MASHINDANO KAMA HAYA HUWA NI BAHATI NA SIBU. HUYO MNATA NDIO HAELEWI KABISA KUWA KUPOTEZA MUDA KWA GOLI MOJA BADALA YA KUANZISHA MPIRA WATU WAPIGE COUNTER ATTACK WAPATE MAGOLI YA KUTOSHA ILI YAWASAIDIE UGENINI HATA MKIFUNGWA GOLI CHACHE MVUKE HATUA NYINGINE.
NI MTIZAMO TU.