Gef
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 507
- 459
Taasisi ya Jamii Africa kupitia jukwaa lake la JamiiForums @jamiiforums imeandaa mjadala maalum uliowakutanisha wadau kutoka serikalini, asasi za kiraia, pamoja na wananchi, kwa lengo la kujadili na kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa katika jamii.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Programu ya Taasisi ya Jamii Africa Ziada Selukindo
amesema mjadala huo umeangazia namna rushwa inavyoathiri huduma za msingi kama afya, elimu na miundombinu, huku ukitoa nafasi kwa washiriki kueleza uzoefu na mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupambana na janga hilo.
"Lengo letu ni kujenga uelewa wa pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa ni suala linalotuhusu sisi sote kama jamii."