Ziara Rais Samia zinavyotumika kuhalalisha upigaji

Ziara Rais Samia zinavyotumika kuhalalisha upigaji

Punguza usinichi mkuu. Fanya yanayokuhusu......... Mengine temana nayo.



Tutakutimbia na kluza huko ziwani, Kaa mbali.
Yaani fedha za Watanzania zinatumika vibaya wewe na kibyongo chako unaita usinichi?
 
Unauhakika kuwa ww ni mwandishi wa habar?
Acha kutungua story mm npo hapa hayo unayasema ni uongo mtupu

sema tu umeumizwa na nyomi la watu kwenye ziara ya Mh. Rais wetu mpendwa Dr Samia Suluhu Hassan
Hata panaposemwa hupajui Ila Uchawa unakusumbua. Acha TAKUKURU wafanye kazi uongo wangu utadhihirika.
 
Asubuhi ya Leo majira ya saa 5 hivi nimepishana na msafara wa Rais ukitokea mkoa wa Rukwa kuelekea Songwe. Binafsi kama Mwandishi wa habari za mazingira naelekea mwambao wa ziwa Tanganyika kikazi. Nilipofika Namanyere wilaya ya Nkasi nimeachana na basi niliyokuja nayo toka Mbeya maana inaendelea na Safari Hadi Mpanda Katavi nami kikazi naelekea tarafa ya KIRANDO hivyo nalazimika kuchukua usafiri mwingine kuelekea huko.

Wakati nasubiri usafiri hapa stendi Kuu Namanyere nimekutana na Stori ya ajabu ambayo sijawahi kuisikia maeneo mengine. Vijana wa Bodaboda na wapiga Debe wanahadithiana Jambo ambalo limefanyika hapa jirani na Stendi usiku wa July 14 kuamkia July 15 siku ambayo Rais Samia alianza ziara Mkoani Rukwa akitokea Katavi.

Kwamba tarehe 14 Julai kwenye kiwanja cha Wazi karibu na Stendi kilifanyika Sherehe iliyobatizwa jina la Mkesha wa Mama ulioandaliwa na viongozi wa Wilaya hii wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya. Katika Mkesha huo wa nje watu walisafirishwa toka Kata zote, kulikuwa na vinywaji vikali na baridi vya kutosha, Muziki wa kukodi, nyama choma ya Mbuzi na Nyamapori na pia waalikwa toka mbali pamoja na Viongozi walilipwa posho na Wageni kulipwa malazi.
Labda wenzangu mnieleze faida ya Aina hii ya mikesha. Yaani Mh. Rais kalala Mpanda, halafu Wananchi wa mkoa mwingine wanakesha wakinywa na kucheza Kwa gharama za serikali? Mh Rais amefika Namanyere akazindua mradi mmoja tu wa Hospitali ya wilaya na akasalimia Wananchi Kwa Muda mfupi Sana. Wengi tuliona maana TBC ilikuwa live. Kwa shughuli hiyo ya nusu saa ya Mh Rais ndo watu wakeshe usiku kucha wakila na kunywa kumsubiri?

Mbona Jambo hili halijafanywa Sumbawanga ambako Rais amelala siku 3 July 15-18?
Hapa hela ya Watanzania imepigwa Kwa Kisingizio cha Mkesha wa kumsubiri Mama.

Hivi ni utamaduni wa kabila gani nchi hii ukisikia kesho mgeni anakuja kwako wewe unalala nje ukila na kulewa na mgeni Huyo kwako anapita tu hata maji hanywi, Maana Mh Rais hakula wala kunywa hapa Namanyere.

TAKUKURU tafadhali, haya ni matumizi mabaya ya fedha za Umma, tunataka kusikia kiasi kilichotumika na kilitoka fungu gani.

Mji hauna maji ya uhakika halafu viongozi wanachukua fedha za Umma kugharamia matukio ya kujineemesha? HAPANA.
Nchi ya kitu kidogo, nchi ya watu wadogo.
 
Kodi yenyewe leo umelipa sh ngapi mkuu
Nimekunywa kahawa vikombe viwili kwa sh elfu 12. Nina risiti ya kielectronik. Kodi nyingine kubwa nalipa tarehe 20. Halafu mje kulialia haitoshi sababu ya kupigapiga misele na kula na kula
 
unajua tz yetu ni nchi ya ajabu sana,na ina watu wa ajabu sana,maisha yao wameyaingiza kwenye ushabiki as if kama majuha,maisha ni magumu,watu wanauliwa ovyo,watu wanapanga sheria kandamizi juu yao na watoto wao bado wanawashangilia tu
anyway ngoja tuendelee kuishi
 
Back
Top Bottom