Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZIARA TARAFA YA LIGANGA, KATA YA LUGARAWA- KIJIJI CHA MDILIDILI- SHULE YA SEKONDARI LUGARAWA.
Februari 23, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walifanya kikao na wananchi wa Kata ya Lugarawa juu ya majanga ya moto yaliyo tokea Februari 14 na 21, 2023 katika mabweni ya Shule ya Sekondari Lugarawa.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya alipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati wa bweni la wanafunzi wa kiume shuleni hapo; baada ya Ushirikiano baina Ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya; Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mbunge wa Jimbo la Ludewa na Wananchi waliojitolea ili kukarabati Bweni hilo Baada ya ajali ya moto Tarehe 14 Feb 2023- hadi sasa kasi ya ukarabati inaridhisha na Wanafunzi watarejea kwenye matumizi ya bweni hilo hivi punde.
Pia amepokea taarifa za jaribio la kuchoma bweni la watoto wa kike lililofanyika Februari 21, 2023 na kupelekea kuungua kwa magodoro matatu, shuka na blanketi lakini uharibifu wa miundombinu uliotokea katika harakati za kuuzima huo moto.
Mkuu wa Wilaya ameelekeza Idara ya zima moto Wilaya kutoa Elimu mashuleni na kwa wananchi juu ya namna ya kupambana na majanga ya moto.
Amewaomba Wananchi na wanafunzi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama, sambamba na kamati iliyo undwa kuchunguza majanga hayo ili kubaini vyanzo vya moto; na wahusika kutokana na ushaidi na viashiria husika.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewaasa wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo yao ili wanendelee kufanya vyema ngazi ya Mkoa na Taifa kwa ujumla. Kwani mojawapo ya ajenda kuu ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka ni Elimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan- ameonesha dhamira ya kuendelea kuboresha Taaluma nchini- kwa Kuongeza Bajeti za miundombinu ya Elimu hivyo ni wajibu wa wananchi kutunza miundombinu hiyo kwani ni uwekezaji Wenye manufaa kwa jamii.
Mkutano huu wa umma ulitoa nafasi ya wananchi kuwasikiliza na viongozi wao ngazi mbalimbali na kwa umuhimu zaidi kutoa maoni yao, maono yao, ushauri wao yote katika kustawisha Taaluma na maendeleo ya jamii kiujumla.