Ziara ya Diamond barani Ulaya kumuingizia takriban shilingi milioni 100

Ziara ya Diamond barani Ulaya kumuingizia takriban shilingi milioni 100

heaven on desert

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
1,025
Reaction score
393
Hivi karibuni Diamond Platnumz
alilazimika kuahirisha ziara yake ya
barani Ulaya baada ya waandaaji
kushindwa kukamilisha kumlipa
hela yake ya advance katika muda
muafaka.
Inadaiwa kuwa katika ziara hiyo
Diamond alitakiwa kulipwa dola
50,000 ambazo ni takriban shilingi
milioni 80 za Kitanzania na
ameithibitishia Bongo5 kuwa ni
kweli japo kuna taarifa kuwa kiasi
hicho alikikataa.
Ameiambia Bongo5 kuwa ziara hiyo
itafanyika mwezi ujao ambapo
baada ya ziara hiyo atarudi
nyumbani na kisha kwenda tena
kwaajili ya nyingine. Kutokana na
makubaliano mapya ya ziara hiyo
kuna uwezekano wa ziara hiyo ya
kwanza kumuingizia karibu shilingi
milioni 100 ama zaidi.
Jumamosi hii Diamond alilazimika
kutumia website yake kutoa taarifa
ya kuahirisha kwa ziara hiyo.
“Kutokana na kampuni ya United
Events Ltd Tilburg-The Netherlands
kwa upande mwingine kama
promoter kushindwa kutimiza
baadhi ya mahitaji ikiwemo
kushindwa kulipa pesa ya show
ambayo ilitakiwa ifanyike
Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/
Germany 09/03/2013 na zingine
kama East African Night ambayo
ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/
Holland tarehe 15/03/2013 na
kadhalika, mimi na team yangu
nzima ya wasafi hatutoweza
kuhudhuria kwenye events hizo,”
alisema.
“Nilikuwa nikipata maswali mengi
sana toka kwa mashabiki zangu
mbalimbali wakiniuliza kuhusiana
na ujio wangu wa nchi hizo za
EUROPE lakini siku zote nilikua
kimya sikuweza kujibu wala
kuzungumza chochote na wadau
wangu kutokana na kutokuwa na
uhakika wa tour hiyo.”
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1362995724984.jpg
    uploadfromtaptalk1362995724984.jpg
    122.8 KB · Views: 204
Washajua kama anatumia ndumba na ndio mana wakahailisha

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ulaya hatapata sifa kwani miondoko yake haijakaa kiAfrika labda avae ngozi na apige ngoma
 
Hivi karibuni Diamond Platnumz
alilazimika kuahirisha ziara yake ya
barani Ulaya baada ya waandaaji
kushindwa kukamilisha kumlipa
hela yake ya advance katika muda
muafaka.
Inadaiwa kuwa katika ziara hiyo
Diamond alitakiwa kulipwa dola
50,000 ambazo ni takriban shilingi
milioni 80 za Kitanzania na
ameithibitishia Bongo5 kuwa ni
kweli japo kuna taarifa kuwa kiasi
hicho alikikataa.
Ameiambia Bongo5 kuwa ziara hiyo
itafanyika mwezi ujao ambapo
baada ya ziara hiyo atarudi
nyumbani na kisha kwenda tena
kwaajili ya nyingine. Kutokana na
makubaliano mapya ya ziara hiyo
kuna uwezekano wa ziara hiyo ya
kwanza kumuingizia karibu shilingi
milioni 100 ama zaidi.
Jumamosi hii Diamond alilazimika
kutumia website yake kutoa taarifa
ya kuahirisha kwa ziara hiyo.
"Kutokana na kampuni ya United
Events Ltd Tilburg-The Netherlands
kwa upande mwingine kama
promoter kushindwa kutimiza
baadhi ya mahitaji ikiwemo
kushindwa kulipa pesa ya show
ambayo ilitakiwa ifanyike
Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/
Germany 09/03/2013 na zingine
kama East African Night ambayo
ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/
Holland tarehe 15/03/2013 na
kadhalika, mimi na team yangu
nzima ya wasafi hatutoweza
kuhudhuria kwenye events hizo,"
alisema.
"Nilikuwa nikipata maswali mengi
sana toka kwa mashabiki zangu
mbalimbali wakiniuliza kuhusiana
na ujio wangu wa nchi hizo za
EUROPE lakini siku zote nilikua
kimya sikuweza kujibu wala
kuzungumza chochote na wadau
wangu kutokana na kutokuwa na
uhakika wa tour hiyo."
Naona jumatatu imefika sasa, ushaingia ofisini kwako tayari! Vipi na chupi za diamond umekumbuka kuzifua au umekimbilia tu JF??
 
Jibu limfaalo mjinga ni kupiga kimya,kwanini msimpigie kimya tu?
 
Bab show za ulaya hazilipi kama show za nyumbani!....ukiona diamond anapiga hela nje jua mkono wa hariry upo na si mziki!..
 
Who is diamond in europe.milioni 100 kwa watu gani watakaoingia?km ni sisi wabeba box sijui kwa kiingilio kipi,maana mbeba box kiingilio anachomudu si zaidi ya dola 20.
 
Back
Top Bottom