Hilaaliy
New Member
- Apr 8, 2024
- 3
- 1
Nasema hili kwa maana kwamba tuna tatizo la umeme mwezi mzima eneo letu, hakuna huduma ya umeme, na tushafanya ufuatiliaji wa njia zote pale Mkuranga, majibu ni kuwa tusubiri suala letu liko ngazi ya juu ya ufundi, lakini hawajawarudishia majibu ya nini kifanyike kutatua changamoto hiyo na wala hukuna kilichoboreshwa.
Pale kituo cha huduma kwa wateja hata unapotoa namba ya taarifa ya mwezi uliopita wala hawashituki kwani majibu unayopewa ni kama mtoa taarifa wa leo tu kwamba tunawasiliana na mafundi wetu watakufikieni kutatua changamoto yenu.
Hatujui mafundi hao ni kutoka hapo Mkuranga au mafundi wengine kutoka nje ya nchi maana kama ni kutoka Mkuranga huu ni mwezi majibu ni kufikiwa na mafundi.
TANESCO ikifa mimi siwezi kulia, nitaitupa Ruvu iwe chakula cha mamba!