Ziara ya Ernesto Che Guevara Tanzania

Ziara ya Ernesto Che Guevara Tanzania

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Wana Jf,

Je? Nikweli mwanamapinduzi wa Kikuba (Ki-Cuba) mwenye asili ya Argentina, Ernesto Che Guevara amewahi kuzuru Tanzania zaidi ya mara moja na je? Lengo lilikuwa ni nini?

attachment.php

Attachments

  • 943527_188629394636366_417269782_n.jpg
    943527_188629394636366_417269782_n.jpg
    56.4 KB · Views: 6,903
Last edited by a moderator:
Sikuwahi kusikia kwamba alifika Tz ingawa alifika Kongo (Zaire) na kusaidia harakati za kivita.
 
Alikwenda kongo kupitia Tanganyika ilibidi arudi zake cuba bila kufanikisha kilichomleta kwa sababu wakongoman kama walivyo watanzania wa leo walipenda kufanya ngono zaidi kuliko kupigana na mkoloni.
 
hmna alishwahi kufika sema cjajua alikuja kwa ajili gani....
 
Che Guevara[John the Baptist] alifika Kigoma with 100 Cuban Revolutinaries. Lakini alisikitika sana kuona kwamba Waaafrika hawana mwamko wa kisiasa,akaondoka. Alikuja kwa madhumuni ya Kwenda Kongo. Halafu akaenda Bolivia,akauawa,akakatwa kichwa. Alipokuwa Dar es Salaam,nasikia favourite restaurent yake ilikuwa ni Zahir Hotel. Hii Zahir Hotel sijui kama bado ipo. Nimewahi kwenda pale siku moja kula biriyani.
 
Ni kweli Che alikuja Tz 1964 akitokea Congo, ni kweli pia wapiganaji wa Congo walimkatisha tamaa kwa sababu kila ikifika jioni ni lazima wapate pombe, muziki na ngono.

Lakini wapiganaji hao wa Congo walimpenda sana kutokana na ujasiri na umahiri wake wa mapambano, wakati anawaaga kwenda kwenye mapambano ya Bolivia walimpa kifurushi cha Almasi ili zikamsaidie kwenye mapambano ya Bolivia, lakini alikataa akawaambia "SIKUJA KUFANYA BIASHARA, NIMEKUJA KUPIGANA!" Alipotoka huko alipitia Dar, alikaa siku chache kabla kuelekea Bolivia alikokwenda kuuawa kikatili na CIA ya Marekani.

Manowari ya Kimarekani iliegeshwa katika bahari ya Hindi katika fukwe za Tz zikiwa na vifaa maalum vya kumfuatilia nyendo zake ili kumnasa na kumuua, lakini msimamo wa Nyerere ulikuwa pamoja na wapigania uhuru hivyo hakuwapa ushirikiano wamarekani kabisa katika suala hilo (alikuwa kwenye orodha ya magaidi pamoja na kina Nelson Mandela kwa mtazamo wa Marekani) Hivyo Comrade Che Guevara alijisikia nyumbani alipokuwa Dar, hivyo inawezekana kabisa alikwenda kula biriyani pale Zahir Restaurant.

Marekani haikuunga mkono mapambano ya ukombozi dhidi ya Wakoloni, na mpaka leo Marekani haiungi mkono mapambano yoyote ya kujikomboa kiuchumi, hasa kwa nchi ndogo zenye rasilimali nyingi ambazo wao wanazihitaji, watazidumaza kwa misaada na kuwahonga viongozi wake ili zisijitegemee ili zisiwe na maamuzi yake yenyewe juu ya rasilimali hizo, bali maamuzi yawe ni yao wamarekani, ndivyo ilivyo kwetu Tz, hatutakuwa na maamuzi juu ya Gesi wala Urani yetu, hata wananchi wakipinga nguvu za ziada za kijeshi zitatumika dhidi yao, lakini kule South Africa kwa Mzee Madiba hali ni tofauti, viongozi wa Marekani hawapati mapokezi mazuri kutoka kwa wananchi zaidi ya yale ya kiserikali, rasilmali zao wanazipangia wenyewe, hata Obama hawakumshobokea bali waliandamana kupinga ujio wake na walitaka akamatwe na kushtakiwa kwa kukiuka haki za binadamu kunakofanywa na utawala wake sehemu mbalimbali duniani, hata familia ya Mzee Mandela ilimkatalia kwenda kumjulia hali Mzee Mandela hospitalini.

Che Guevara angekuwa hai leo, au kama huko aliko anaweza kutuona tunavyowashobokea Wamerakani, hakika angetulaani na kutuchukia kuliko alivyowachukia wapiganaji wa Congo!
 
Che Guevara[John the Baptist] alifika Kigoma with 100 Cuban Revolutinaries. Lakini alisikitika sana kuona kwamba Waaafrika hawana mwamko wa kisiasa,akaondoka. Alikuja kwa madhumuni ya Kwenda Kongo. Halafu akaenda Bolivia,akauawa,akakatwa kichwa. Alipokuwa Dar es Salaam,nasikia favourite restaurent yake ilikuwa ni Zahir Hotel. Hii Zahir Hotel sijui kama bado ipo. Nimewahi kwenda pale siku moja kula biriyani.

Zahir Hotel bado ipo.
 
Alikuja Tanzania alikaa kule Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kufanya mambo hapo Congo.
 
Zahir Hotel bado ipo.
Mkuu Ritz nijuze ilipo hii hotel ili nikapate msosi pale may be naweza kuotea na kukaa the same area ambayo Comrade Che Guevara alikaa....hata nikikosea eneo sio issue as far as i believe entrance haijabadilika.
 
Last edited by a moderator:
ni kweli comrade
"che" alifika tz mwaka 1964, mwanzoni aliomba kwenda kuwasaidia FRELIMO wa msumbiji lakini mambo hayakukaa sawa(ninayo picha ya che akiwa na mondlane kwenye kikao hapa dsm ila sina ujuzi wa kuiweka hapa) baadae akasafiri kwa gari all the way to kigoma then to zaire to assist kabila (sinior)katika harakati za ukombozi. hakukaa sana kule akarudi dsm na kutulia pale ubalozi wa cuba kwa takribani miezi miwili akiandika war diaries. akiwa dar aliweza kusafiri kwenda zanzibar kukutana na macomrade wa kule.
che amekufa kimwili ila kifikra na kimtizamo bado yuko hai
 
Alikwenda kongo kupitia Tanganyika ilibidi arudi zake cuba bila kufanikisha kilichomleta kwa sababu wakongoman kama walivyo watanzania wa leo walipenda kufanya ngono zaidi kuliko kupigana na mkoloni.

Hahaa! Kaka kweli umetuchoka - ndivyo tulivyo Watz wa leo?
 
ni kweli alishawahi kufika tanzania, katika wanamapinduzi waliomoyoni mwangu che guevara ni namba moja..... nina barua yake aliyokuwa anamuaga Fidel castro wa Cuba wakati anajitoakwenye Serikali ya Cuba kuelekea Congo kupitia hapa Tanzania , kwakweli Baba wa Taifa alikuwa jembe lisilokumbatia ukoloni na unyonyaji.
 
Alikwenda kongo kupitia Tanganyika ilibidi arudi zake cuba bila kufanikisha kilichomleta kwa sababu wakongoman kama walivyo watanzania wa leo walipenda kufanya ngono zaidi kuliko kupigana na mkoloni.

huko Congo alishindwana na Kabila (Senior) kwani aliona hana nia ya kweli kupigania unyonyaji. akasepa kuelekea Bolivia ambapo mauti yalimkuta ,RIP kamanda mitazamo yako tumejifunza hata sisi kizazi ambacho hatujakushuhudia.
 
Kuna habari zinazosema kuwa Che na Castrol walikosana. Castrol akataka Che aondoke Cuba. Hivyo alivyosafiri, Castrol akaandika barua kama vile ni CHE ameandika ili kuwaaga watu wa Cuba kuwa hatarudi tena Cuba.

Hiyo ilipelekea jamaa kuanza kutangatanga hapa na pale. Maada ya kutoka Tanganyika, kuna kila dalili kuwa mipango yake ilikuwa imekaa ovyo na kwa hali ya kawaida, angelitaka kurudi NYUMBANI ambako ilikuwa CUBA. Ila kutokana na barua hiyo, ikawa ameshafungiwa tayari milango. Akaondoka kichwakichwa kuelekea Bolivia ambako hawa Wajinga wakiwa wameshapewa habari kuwa yupo pale kijijini kwao hoi, wakaenda na kumuuwa. Nasikia baadaye walijilaani sana kugunduwa wametumika kumuuwa mtu kama huyo.

ni kweli alishawahi kufika tanzania, katika wanamapinduzi waliomoyoni mwangu che guevara ni namba moja..... nina barua yake aliyokuwa anamuaga Fidel castro wa Cuba wakati anajitoakwenye Serikali ya Cuba kuelekea Congo kupitia hapa Tanzania , kwakweli Baba wa Taifa alikuwa jembe lisilokumbatia ukoloni na unyonyaji.
 
Last edited by a moderator:
Alikuja Zanzibar kwa Mwaliko wa Comrades na alihutubia na kwenye KIRIRI alipanda pia Col. Ali Mahfoudh Mwanafunzi wake
 
Mkuu Ritz nijuze ilipo hii hotel ili nikapate msosi pale may be naweza kuotea na kukaa the same area ambayo Comrade Che Guevara alikaa....hata nikikosea eneo sio issue as far as i believe entrance haijabadilika.

Mkuu NasDaz,

Hipo Mosque Street wala haijabadikika sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom