asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,035
Kuna habari zinazosema kuwa Che na Castrol walikosana. Castrol akataka Che aondoke Cuba. Hivyo alivyosafiri, Castrol akaandika barua kama vile ni CHE ameandika ili kuwaaga watu wa Cuba kuwa hatarudi tena Cuba.
Hiyo ilipelekea jamaa kuanza kutangatanga hapa na pale. Maada ya kutoka Tanganyika, kuna kila dalili kuwa mipango yake ilikuwa imekaa ovyo na kwa hali ya kawaida, angelitaka kurudi NYUMBANI ambako ilikuwa CUBA. Ila kutokana na barua hiyo, ikawa ameshafungiwa tayari milango. Akaondoka kichwakichwa kuelekea Bolivia ambako hawa Wajinga wakiwa wameshapewa habari kuwa yupo pale kijijini kwao hoi, wakaenda na kumuuwa. Nasikia baadaye walijilaani sana kugunduwa wametumika kumuuwa mtu kama huyo.
aksante mkuu Sikonge ,ila niliwahi kuhudhuria kongomano la maadhimisho kama sikosei ya miaka 40 toka che guevara apite Tanzania lilifanyikia UDSM yalihudhuriwa na wanamapinduzi wengi sana na wanahistoria wengi mpaka balozi wa cuba aliyepigana na che wakati wa mapinduzi hayo na ushuhuda wa kitabu cha yule mwanamapinduzi wa zanzibara anaitwa Babu ila sikuwahi kusikia kitu kama hicho cha kugombana na Fidel.
Last edited by a moderator: