Ni kweli Che alikuja Tz 1964 akitokea Congo, ni kweli pia wapiganaji wa Congo walimkatisha tamaa kwa sababu kila ikifika jioni ni lazima wapate pombe, muziki na ngono.
Lakini wapiganaji hao wa Congo walimpenda sana kutokana na ujasiri na umahiri wake wa mapambano, wakati anawaaga kwenda kwenye mapambano ya Bolivia walimpa kifurushi cha Almasi ili zikamsaidie kwenye mapambano ya Bolivia, lakini alikataa akawaambia "SIKUJA KUFANYA BIASHARA, NIMEKUJA KUPIGANA!" Alipotoka huko alipitia Dar, alikaa siku chache kabla kuelekea Bolivia alikokwenda kuuawa kikatili na CIA ya Marekani.
Manowari ya Kimarekani iliegeshwa katika bahari ya Hindi katika fukwe za Tz zikiwa na vifaa maalum vya kumfuatilia nyendo zake ili kumnasa na kumuua, lakini msimamo wa Nyerere ulikuwa pamoja na wapigania uhuru hivyo hakuwapa ushirikiano wamarekani kabisa katika suala hilo (alikuwa kwenye orodha ya magaidi pamoja na kina Nelson Mandela kwa mtazamo wa Marekani) Hivyo Comrade Che Guevara alijisikia nyumbani alipokuwa Dar, hivyo inawezekana kabisa alikwenda kula biriyani pale Zahir Restaurant.
Marekani haikuunga mkono mapambano ya ukombozi dhidi ya Wakoloni, na mpaka leo Marekani haiungi mkono mapambano yoyote ya kujikomboa kiuchumi, hasa kwa nchi ndogo zenye rasilimali nyingi ambazo wao wanazihitaji, watazidumaza kwa misaada na kuwahonga viongozi wake ili zisijitegemee ili zisiwe na maamuzi yake yenyewe juu ya rasilimali hizo, bali maamuzi yawe ni yao wamarekani, ndivyo ilivyo kwetu Tz, hatutakuwa na maamuzi juu ya Gesi wala Urani yetu, hata wananchi wakipinga nguvu za ziada za kijeshi zitatumika dhidi yao, lakini kule South Africa kwa Mzee Madiba hali ni tofauti, viongozi wa Marekani hawapati mapokezi mazuri kutoka kwa wananchi zaidi ya yale ya kiserikali, rasilmali zao wanazipangia wenyewe, hata Obama hawakumshobokea bali waliandamana kupinga ujio wake na walitaka akamatwe na kushtakiwa kwa kukiuka haki za binadamu kunakofanywa na utawala wake sehemu mbalimbali duniani, hata familia ya Mzee Mandela ilimkatalia kwenda kumjulia hali Mzee Mandela hospitalini.
Che Guevara angekuwa hai leo, au kama huko aliko anaweza kutuona tunavyowashobokea Wamerakani, hakika angetulaani na kutuchukia kuliko alivyowachukia wapiganaji wa Congo!