Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZIARA YA KATIBU MWENEZI ZANGINA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA, MALINYI
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Ndugu Zangina S. Zangina katika kipindi cha Kujiandikisha alitumia muda mwingi kuhamasisha Wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji zoezi lililoanza tarehe 11 Oktoba, 2024 na kutamatika tarehe 20 Oktoba, 2024
Katibu Mwenezi Zangina kwa kushirikiana na Katibu wa CCM Wilaya ya Malinyi, Bingwa Abdul Hamad (Dogo) alifika Wilaya ya Malinyi katika Kata ya Malinyi Kijiji cha Makerere, Kijiji cha Mchangani na Kijiji cha Malinyi (Makugila B na Makugila Madukani) ambapo alikutana na Mabalozi, Viongozi wa Matawi na wa Kata ili kuwapa Elimu na Mbinu kuhamasisha na kutia msukumo kwa zoezi la Uandikishaji.
Akiwa Malinyi, Komredi Zangina aliendelea kutoa elimu ya mbinu za kuongeza idadi ya Wanaojiandikisha, alifika Kata ya Ngoheranga, Kijiji cha Tanga na kufanya kikao cha ndani cha Mabalozi, Wenyeviti wa Vijiji, Viongozi wa Matawi na Kata kisha alifika kituo cha Uandikishaji cha Kitongoji cha Tanga A, Tanga B, Uzunguni, Ngoheranga, Madukani.
Aidha, Komredi Zangina alitumia fursa hiyo akiwa Kitongoji cha Ngoheranga kuzungumza na mmoja wa viongozi wa Msikiti ambaye ni Mwenyekiti Teuka Kyadulaga juu ya Ombi la kuwatangazia waumini na majirani juu ya kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi na Mwenyekiti wa Msikiti alipokea Ombi kwa mikopo miwili.
Mwisho, Zangina S. Zangina alihihitimisha ziara yake Malinyi kwa kufanya Kikao kilichokutanisha Vitongoji vya Lupunga na Ngojeranga ambapo alikutana na Mabalozi, Wenyeviti wa Vijiji na Viongozi wa Matawi ili kutoa elimu na mbinu ya jinsi gani waongeze idadi ya watu wanaojiandikisha, ambao walifurahia sana kwa elimu na mbinu hizo kupitia kikao hicho.
Attachments
-
WhatsApp Video 2024-10-23 at 17.32.21.mp418.5 MB
-
WhatsApp Video 2024-10-23 at 17.32.36.mp46.1 MB
-
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.29.12.jpeg118 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.30.25.jpeg130.6 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.30.25(1).jpeg114.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.32.55.jpeg149 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.33.59.jpeg135.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.34.29.jpeg97.4 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.35.26.jpeg112.7 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.35.43.jpeg94.4 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.36.03.jpeg81.7 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-10-23 at 17.36.38.jpeg124.5 KB · Views: 5