Ziara ya Mbunge Jimbo la Babati Vijijini

Ziara ya Mbunge Jimbo la Babati Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. DANIEL BARAN SILLO AFANYA ZIARA KATIKA JIMBO LA BABATI VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daniel Baran Sillo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ameendelea na ziara katika Jimbo lake la Babati Vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Mhe. Daniel Sillo Mbunge wa Babati Vijijini tarehe 30/4/2023 alitembelea Gate linalojengwa la kuingia hifadhi za Taifa ya Tarangire kupitia Mamire ambapo pia zimepatikana fedha za kujenga daraja na barabara ya kuingia hifadhini.

Mhe. Daniel Sillo Mbunge wa Babati Vijijini tarehe 30/4/2023 alikagua mradi wa Maji wa Kijiji cha Hoshan Kata ya Duru ambapo pia alitoa Jezi kwa timu ya mpira ya Kijiji cha Hoshan

Vilevile, Mbunge wa Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo tarehe 1/5/2023 alikabidhi Kompyuta (Computer) katika Shule ya Sekondari ya Ufana iliyopo Kata ya Secheda ili iwasaidie kujifunza somo la ICT (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano)

Aidha, Mbunge wa Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo tarehe 1/5/2023 alifanya ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kijiji cha Orbesh katika Kata ya Secheda pia alitoa jezi kwa timu za kijiji cha Orbesh.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.41.jpeg
    36.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.43(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.43(1).jpeg
    44.5 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.44(1).jpeg
    38.2 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.46(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.46(1).jpeg
    50.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 16.02.44.jpeg
    69.5 KB · Views: 7
Back
Top Bottom