Ziara ya Nancy Pelosi nchini Taiwan ilitoa jibu

Ziara ya Nancy Pelosi nchini Taiwan ilitoa jibu

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
Raisi Xi wa China alitoa vitisho kuhusiana na ziara ya bi Perosi nchini Taiwan. Wote tulisikia. Pamoja na vitisho vyote, Marekani wakapuuza, bi mkubwa akaingia Taiwan. Wote tuliona, mchana kweupe.

Wote tulifuatilia msafari wa bi Perosi. Ndege, meli za kivita zilikuwa zimeizunguka Taiwan, lakini Yule Bibi akaingia na kutoka kwa ujasiri na kejeli kubwa. Mchina aliishia kurusha mabomu baharini.

Marekani alikuwa anatufundisha kwamba MChina hana chochote kwake.

Taiwan bado imeshikiliwa na Marekani, wa China wanafanya drills miaka nenda rudi. Cha ajabu tunajizima data, HATUJIFUNZI.

MChina bado Sana, Sana, Sana. Ana miaka zaidi ya 200 na asipoangalia, hawezi kuitawala dunia.
 
,kama huyo USA asingekuwa anamuogopa Mchina kuna haja gani ya kuushikilia mgogoro kati ya China na Taiwan?
Mgogoro huo USA anautumia kama kete sababu amefanya calculations zake aakajua kuwa ipo siku China atahatarisha nafasi yake ya ukitanja wa Dunia-hivyo anatumia Taiwan kama kete ili China asifanikiwe.
 
Raisi Xi wa China alitoa vitisho kuhusiana na ziara ya bi Perosi nchini Taiwan. Wote tulisikia. Pamoja na vitisho vyote, Marekani wakapuuza, bi mkubwa akaingia Taiwan. Wote tuliona, mchana kweupe.

Wote tulifuatilia msafari wa bi Perosi. Ndege, meli za kivita zilikuwa zimeizunguka Taiwan, lakini Yule Bibi akaingia na kutoka kwa ujasiri na kejeli kubwa. Mchina aliishia kurusha mabomu baharini.

Marekani alikuwa anatufundisha kwamba MChina hana chochote kwake.

Taiwan bado imeshikiliwa na Marekani, wa China wanafanya drills miaka nenda rudi. Cha ajabu tunajizima data, HATUJIFUNZI.
MChina bado Sana, Sana, Sana. Ana miaka zaidi ya 200 na asipoangalia, hawezi kuitawala dunia.
Hakuna anayetaka vita reja reja. Siku kadhaa mrusi kapitisha subs zake karibu na pwani ya Marekani akielekea Cuba. Umesikia wamarekani wako worried, lakini hawazitungua ama kuingia vitani. Funzo ni kwamba hakuna anayetaka vita reja reja ambavyo anajua hata akivishinda vitamgharimu.
 
Ebu fikiria kama Iran ikiweza ku control ule upande (maana kwa upande huo yeye ndio mwenye resources nyingi),Russia aziweke Nchi za Ulaya kwapani ( maana Russia ndio anaongoza kwa resources Duniani),na China naye ndio huyo anampumlia kwapani USA.
Unadhani huo U super power wa USA utakuwepo?,ndio maana anafanya juu chini kila upande usipatane.
 
Uzuri ni kuwa wachina wana akili nyingi sana kushinda wewe, wenda kushinda viongozi wako hata wamarekani.

Usifikiri Xi Jinping ana akili kama zako au kama za wamarekani.

Na nina hakika wachina wangekuwa hata na nusu ya akili zako China isingefikisha zaidi ya miaka 5000 mpaka leo ingekuwa imeparanganyika.

Na hilo tukio la Nancy Pelosi wangefanya maamuzi ya mihemko ya hovyo ambayo hayafai.

Kuwa kiongozi China sio rahisi kama kuwa kiongozi katika nchi yako kwamba mtu mjinga yoyote anaweza pewa madaraka ya kuongoza taifa.

Issue ya Taiwan ni issue sensitive sana kwa wachina kuliko unavyo fikiri na ni issue muhimu sana kwa wa marekani unahitaji viongozi wenye akili sio wanasiasa walio jaa mihemko.

Nakukumbusha China ni taifa kubwa sana linalo pambana na marekani katika kila nyanja unaoijua wewe hapa duniani, changanya za kwako halafu jiulize ule uamuzi wa China ni sahihi au si sahihi.

By the way wachina wana mission 2025, 2035 na 2049 kasome hizo mission ujue wachina nini wanataka hapa duniani.

Mpaka kufika 2049 nina uhakika wa 100% issue ya Taiwan itakuwa solved let's wait and see.
 
Ubaya ni kuwa wachina wana akili nyingi sana kushinda wewe, wenda kushinda viongozi wako hata wamarekani.

Usifikiri Xi Jinping ana akili kama zako au kama za wamarekani.

Na nina hakika wachina wangekuwa hata na nusu ya akili zako China isingefikisha zaidi ya miaka 5000 mpaka leo.

Na hilo tukio la Nancy Pelosi wangefanya maamuzi ya mihemko ya hovyo ambayo hayafai.

Kuwa kiongozi China sio rahisi kama kuwa kiongozi katika nchi yako kwamba mtu mjinga yoyote anaweza pewa madaraka ya kuongoza taifa.

Issue ya Taiwan ni issue sensitive sana kwa wachina kuliko unavyo fikiri na ni issue muhimu sana kwa wa marekani unahitaji viongozi wenye akili sio wanasiasa walio jaa mihemko.

Nakukumbusha China ni taifa kubwa sana linalo pambana na marekani katika kila nyenzo unaoijua wewe hapa duniani, changanya za kwako halafu jiulize ule uamuzi wa China ni sahihi au si sahihi.

By the way wachina wana mission 2025, 2035 na 2049 kasome hizo mission uje wachina nini wanataka hapa duniani.

Mpaka kufika 2049 nina uhakika wa 100% issue ya Taiwan itakuwa solved let's wait and see.
Hata kama atapewa miaka 100 Hilo tatizo hawezi.
 
Hizi nchi tajiri vikao vyao ni namna ya kugawana resources za nchi maskini...
Wanakuchanganya tu hawana ugomvi wowote...
DRC nani?
USA: Nipeni mimi hapo
China: Mimi nitawauzia waasi silaha
TZ nani?
USA: pale tugawane wote,
Zambia nani?
USA: China utamalizana nao
RUSSIA: Mimi naomba niwachukue hawa waliopindua uongozi.
n.k ndio huwa mada zao hizo
 
Hata kama atapewa miaka 100 Hilo tatizo hawezi.
Uzuri ni kuwa wachina wana akili nyingi kushinda wewe na wame experience mambo mengi katika historia yao kushinda wewe na wana viongozi wanaojitambua na kuitambua China kushinda wewe.

Wewe hapo nikikuambia ufungue tu historia ya nyuma ya miaka 100 ya taifa lako sijui kama utaweza au hata taifa lako litakuwepo.

Kama unafikiri Taiwan ndio mgogoro mkubwa wa kwanza kwa wachina wenda ufahamu kuhusu pasua kichwa ya wa Mongol au hata Issues za Macau, Hongkong, Tibet, Xinjiang

Na pia sina hakika hata mgogoro wa Taiwan unaufahamu umekaaje kaaje.

Uzuri China wana viongozi sio wanasiasa. wanajua jana ya China leo ya China ipoje na kesho ya China inapaswa kuwaje
 
Back
Top Bottom