M
MegaPyne
Guest
MADAI YA MALIPO YA WALIMU NCHINI
JK: Ama hatuna ufanisi kabisa
ama tumekuwa wadanganyifu
Na Mwandishi Maalum, Tabora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa madai yasiyoisha ya malipo mbalimbali ya walimu nchini yanathibitisha kuwa baadhi ya viongozi ama wana ukosefu wa kiwango kikubwa cha ufanisi ama ni wadanganyifu.
Ama sisi viongozi ni wakosefu wakubwa wa ufanisi grossly incompetent ama na sisi tumekuwa wadanganyifu - we have simply become cheats. Huwezi mwezi huu ukalipa kiasi cha sh bilioni saba, na miezi mitatu baadaye ukaletewa madai mengine ya sh bilioni 12. Haizekani madeni haya yakawa hayaishi. Hatuwezi kuendelea to run in circles kama wanavyosema Waingereza, amesema Rais Kikwete.
Ameelekeza Rais Kikwete: Jibu la udanganyifu ni kupelekwa kortini na kufungwa tu. Jibu la kukosa ufanisi kwa mtumishi wa umma ni kuondolewa katika nafasi yake na akapatikana mtu mwingine wa kufanya kazi.
Rais ametoa ufafanuzi huo wakati anapokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Tabora katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku nane katika mkoa huo leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2008 mjini Tabora.
Rais alikuwa ameambiwa kuwa walimu katika wilaya hiyo walikuwa bado wanaidai Serikali, hata baada ya kuwa baadhi ya madeni yao yamelipwa.
Ilielezwa kuwa walimu katika wilaya hiyo bado wanaidai Serikali sh milioni 93 ikiwa ni posho ya likizo na za kujikimu, hata baada ya kuwa wamelipwa baadhi ya madai yao Machi, mwaka huu.
Kama nilivyosema juzi Sikonge nataka hili limalizike kwa kufanya ukahiki wa shule kwa shule, mwalimu kwa mwalimu, kichwa kwa kichwa, ili tujue nani hasa anadai nini. Baada ya kupata uhakika huo wale wanaodai tutawalipa, ili tuondokane na madai haya yasiyoisha.
Rais ameongeza: Lazima tukate mzizi wa fitina. Nataka madeni haya yalipwe baada ya kuwa yamehakikiwa. Lazima tumalize misuguano hii. Mwezi Machi tumelipa sh bilioni saba, miezi mitatu baadaye tunaletewa madai mengine ya sh bilioni 12. Sasa nataka hili limemalizike kwa namna ya kudumu, amesema Rais.
Rais ambaye ameonekana kukerwa na hali hiyo amesisitiza: Sasa mwezi Machi tulilipa nini? Hata nyie kama viongozi jiulizeni. Tulimlipa nani, kiasi gani na kwa nini?. Hatuwezi kuendelea na biashara hii bila kuifikisha mwisho.
Kuhusu malalamiko ya uongozi wa wilaya hiyo kuwa hauna nafasi ya kutosha kujenga hospitali ya wilaya, Rais ameelekeza: Nyie viongozi acheni kulalamika na kunungunika. Fanyeni uamuzi. Ama jengeni hospitali ya wilaya katika eneo la wilaya jirani ya Uyui, ama jengeni mjini kwa kupandisha ghorofa kama hamnayo ardhi ya kutosha.
Rais alikuwa ameambiwa kuwa uongozi wa wilaya hiyo unataka kujenga hospitali ya wilaya, lakini hauna ardhi ya kutosha kuweza kujenga hospitali yenye hadhi hiyo.