Ziara ya Rais Masisi: Wakubaliana na Rais Samia kuendeleza Sekta ya Madini na kufufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano

Ina maana yale masoko yetu ya madin ya mkoa Botswana hawana cha kujifunza kweli ?
 
Tunajipambanua kama wapigania Kiswahili lakini elimu yetu bado ipo kwa lugha ya mkoloni. Hayo yote licha ya tafiti juu ya tafiti kuonesha kwamba Kiswahili kina ufanisi zaidi kufundishia katika mazingira yetu na sera yetu ya elimu inataka hivyo.
Unajua hata mkitaka kwenda kufundisha Botswana kiswahili, kigezo cha kwanza ni lazima itabidi ufahamu hiyo lugha unayoita ya mkoloni, ili iweze kuwa rahisi kufundisha hao Watswana....ndo maana nchi za nje nyingi zinazotaka kujifunza kiswahili, wakenya wanakuwa preferred kwa hilo zaidi yetu...bitter truth..
 
Kule wala hawana wachimbaji wadogo...migodi yao especially ya almasi, ni highly machine intensive na goverment wako joint venture na Debeers,ambao ni SA(Mmiliki wa ke ni familia ya Oppenheimer -i.e.ndo walikuwa enzi hizo pale Mwadui)na JV hiyo ya 50/50 inaitwa Debstwana. Hawa jamaa ndo pia wako Namibia kwenye Diamonds na JV vilevile kupitia kampuni inaitwa Namdeb .... jamaa hao wako vizuri maana masoko yako well calculated Kwa wanunuzi wa uhakika... masoko yenu haya sanasana ni kwa wachimbaji wenu wadogo...
 
Botswana kwa Africa wamejitahidi aiseee, na nafikiri pia uwezo wao wa kujaribu kuwa na very strict financial discipline katika mambo karibu yote wanayojaribu kufanya.i.e.iwe ni kwenye sekta ya madini au mifugo au utalii etc. Kwa kweli, kwa level za nchi zetu hizi za kusini mwa jangwa la Sahara, they are among the best....
 
Mstari mmoja unaosema yote ndani ya kurasa mia moja!

Hivi kuna mwaka ambapo tutampata kiongozi ambaye atasimama na kusema "SASA INATOSHA", na kuanza kusimamia hawa watu wote tulionao hapa wafanye kazi na kuleta matokeo yanayoonekana?

Nchi hii haina upungufu wa wataalam katika eneo lolote tunalohitaji litusaidie kuleta maendeleo; bali tuna upungufu mkubwa sana wa kuwasimamia na kuhakikisha wataalam hawa wanatimiza wajibu wao kwelikweli.

Nadhani tunamhitaji kiongozi anayeweza kutumia MABAVU katika eneo hili, kama yale ya Magufuli, bila ya yale mabovu yake mengine.
Mimi nipo tayari kumuunga mkono kiongozi wa namna hiyo wakati huu.
Kumbuka kwamba Huyo mwenye mabavu unayemhitaji naye anamapungufu yake. Ungesema kwamba kuna ttz LA uadilifu katika utumishi wa umma ningekuelewa, so Take it for your own risk.
 
"Kuna upungufu katika utumishi wa umma" - SAWA, ninakubaliana na hili. Huyu mwenye mabavu ninayemtaka, mabavu yake yawe ya huko, "kuondoa upungufu" katika utumishi wa umma. Hayo ndiyo mabavu ninayoyaandika hapa.

Ndiyo, hakuna aliye kamilifu, huyu pia atakuwa na mapungufu yake, ndiyo maana nikaomba yasiwe mapungufu kama aliyokuwa nayo marehemu Magufuli.
 
Unajua hata mkitaka kwenda kufundisha Botswana kiswahili, kigezo cha kwanza ni lazima itabidi ufahamu hiyo lugha unayoita ya mkoloni, ili iweze kuwa rahisi kufundisha hao Watswana....ndo maana nchi za nje nyingi zinazotaka kujifunza kiswahili, wakenya wanakuwa preferred kwa hilo zaidi yetu...bitter truth..
Post yangu nimeongelea elimu yetu na pia sijasema kiingereza hakitafundishwa walau kama somo.
Tunapofanya mabadiliko ya elimu yetu tunafanya kwa manufaa yetu kwanza na sio kwa ajili ya Botswana na Kenya.
 
Ndugu yangu ' kiingereza kwa ulimwengu huu kitaendelea kuwa' muhimu' ,tu na especially kwa sie nchi maskini, ili kuweza kuintegrate ' na kuweza kushindana easily ktk dunia ya leo ambayo imekuwa kijiji sasa. Mabadiliko yoyote utakayofanya katika elimu ni vema ukayaangalia at 'global' dimension strategy ili angalau uweze kutoboa.....narudia, tumechelewa sana....
Post yangu nimeongelea elimu yetu na pia sijasema kiingereza hakitafundishwa walau kama somo.
Tunapofanya mabadiliko ya elimu yetu tunafanya kwa manufaa yetu kwanza na sio kwa ajili ya Botswana na Kenya.
 
Kule wala hawana wachimbaji wadogo...migodi yao especially ya almasi, ni highly machine intensive na goverment wako joint venture na Debeers,ambao ni SA(Mmiliki wa ke ni familia ya Oppenheimer -i.e.ndo walikuwa enzi hizo pale Mwadui)na JV hiyo ya 50/50 inaitwa Debstwana. Hawa jamaa ndo pia wako Namibia kwenye Diamonds na JV vilevile kupitia kampuni inaitwa Namdeb .... jamaa hao wako vizuri maana masoko yako well calculated Kwa wanunuzi wa uhakika... masoko yenu haya sanasana ni kwa wachimbaji wenu wadogo...
😃😃😃 Kwa hiki kiswahil chako ina maana ww ni m botswana ..maaana unasema wachimbaji wetu wadogo
 
Tunajipambanua kama wapigania Kiswahili lakini elimu yetu bado ipo kwa lugha ya mkoloni. Hayo yote licha ya tafiti juu ya tafiti kuonesha kwamba Kiswahili kina ufanisi zaidi kufundishia katika mazingira yetu na sera yetu ya elimu inataka hivyo.

Kama JPM alivyochukua maamuzi magumu kwa kutekeleza viporo vya maamuzi ya tawala za nyuma kama vile; kuhamia Dodoma, kujenga bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, kadhalika Mama Samia naye anaaswa kuweka alama yake kwa kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi zote sambamba na kukitumia mahali popote tunapohusika iwe AU au UN.

Hahitaji kuogopa hata kidogo. Jumuiya ya Ulaya, EU inaundwa na jumla ya nchi 28 miongoni mwao wakiwepo wenye uwezo mkubwa na mdogo kiuchumi. Kwa mujibu wa makubaliano yao, lugha ya kila nchi mwanachama ni "lugha rasmi" kwenye shughuli zote za Jumuiya na hakuna anayelazimika kujifunza lugha ya mwenzake ili eti aitumie kwenye mawasiliano.

Kwa kutambua hayo, ni wajibu wetu Watanzania kuhakikisha kuwa Kiswahili, ambacho kwa sasa kina wazungumzaji takriban milioni 120 na ambacho kinakubalika kama "lingua franca" kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati, kinatumika katika majukwaa na nyanja mbalimbali kitaifa na kimataifa.

Tukumbuke na kuzingatia kuwa "mtegemea cha nduguye, hufa maskini"! Hatutaendelea na kufika tunapotaka kwa lugha ya kuazima kwani siku zote "nguo ya kuazima, haisitiri makalio"
 
Ndugu yangu ' kiingereza kwa ulimwengu huu kitaendelea kuwa' muhimu' ,tu na especially kwa sie nchi maskini, ili kuweza kuintegrate ' na kuweza kushindana easily ktk dunia ya leo ambayo imekuwa kijiji sasa. Mabadiliko yoyote utakayofanya katika elimu ni vema ukayaangalia at 'global' dimension strategy ili angalau uweze kutoboa.....narudia, tumechelewa sana....
Ndugu yangu Bunsen Burner, nakushauri usome historia kidogo kuhusu Waingereza. Utabaini kuwa walitawaliwa na Wafaransa, na katika kutawaliwa huko walioonekana wasomi na wastaarabu ni wale walioweza kuzungumza Kifaransa.

Baada ya mamia ya miaka ya utawala wa Wafaransa, Waingereza walianza kuimarisha lugha yao ambayo leo tunaisujudu kana kwamba ilishushwa na Mungu kila mtu aizungumze.

Soma historia ya Mapinduzi ya Kitamaduni ya China ya mwaka 1949 chini ya Mao Zedong. Walipiga marufuku matumizi ya lugha za kigeni kwenye nchi yao. Waliamua kutumia lugha yao kwenye nyanja zote, na leo kila mmoja wetu ni shahidi wa uamuzi wao ulikowafikisha.

Kwa ufupi ni kwamba, ile lugha unayoitumia uotapo ndoto- ndio lugha iwezayo kuleta mabadiliko katika maisha yako. Je, huwa unaota ndoto kwa Kiswahili au Kiingereza?
 
Mkuu una hoja ya msingi ila hiyo debate ilisha kuwepo muda na ikamalizwa kwa tafiti na facts.

Hizo faida za kiingereza zinaweza kupatikana kwa kusoma kiingereza kama somo (japo hili somo linahitaji mtaala tofauti tukibadili lugha ya kufundishia). Tafuta tafiti za hili suala na utafiti wa serikali juu ya hili.

Kuanza kujadili hilo ni kurudi nyuma. Facts zimeshakuwa established kilichobaki ni utekelezaji.
 
Kama JPM alivyochukua maamuzi magumu kwa kutekeleza viporo vya maamuzi ya tawala za nyuma kama vile; kuhamia Dodoma, kujenga bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, kadhalika Mama Samia naye anaaswa kuweka alama yake kwa kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi zote sambamba na kukitumia mahali popote tunapohusika iwe AU au UN.

Hahitaji kuogopa hata kidogo. Jumuiya ya Ulaya, EU inaundwa na jumla ya nchi 28 miongoni mwao wakiwepo wenye uwezo mkubwa na mdogo kiuchumi. Kwa mujibu wa makubaliano yao, lugha ya kila nchi mwanachama ni "lugha rasmi" kwenye shughuli zote za Jumuiya na hakuna anayelazimika kujifunza lugha ya mwenzake ili eti aitumie kwenye mawasiliano.

Kwa kutambua hayo, ni wajibu wetu Watanzania kuhakikisha kuwa Kiswahili, ambacho kwa sasa kina wazungumzaji takriban milioni 120 na ambacho kinakubalika kama "lingua franca" kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati, kinatumika katika majukwaa na nyanja mbalimbali kitaifa na kimataifa.

Tukumbuke na kuzingatia kuwa "mtegemea cha nduguye, hufa maskini"! Hatutaendelea na kufika tunapotaka kwa lugha ya kuazima kwani siku zote "nguo ya kuazima, haisitiri makalio"
Yaani umeongea kilichokuwa akilini mwangu. Rais Samia akifanikisha hilo atakuwa raisi wangu bora wa muda wote.

Hili ni jambo la msingi ila kila rais anayekuja analipiga danadana kama walivyofanya suala la kuhamia Dodoma na suala la katiba.

Tofauti ya masuala mengine ni kwamba kadri siku zinavyoenda ndivyo tunazidi kutoa wasomi wanakosa kitu fulani cha muhimu.

Pia tunashindwa kuintegrate elimu yetu na utamaduni na mazingira yetu. Ndio maana leo hamna redio wala tv zenye maudhui ya kisayansi wala hautoona riwaya za kitanzania za science fiction. Sisi utakuta tunaongelea uchawi na umbea.
 
Ndugu yangu Bunsen Burner, nakushauri usome historia kidogo kuhusu Waingereza. Utabaini kuwa walitawaliwa na Wafaransa, na katika kutawaliwa huko walioonekana wasomi na wastaarabu ni wale walioweza kuzungumza Kifaransa.

Baada ya mamia ya miaka ya utawala wa Wafaransa, Waingereza walianza kuimarisha lugha yao ambayo leo tunaisujudu kana kwamba ilishushwa na Mungu kila mtu aizungumze.

Soma historia ya Mapinduzi ya Kitamaduni ya China ya mwaka 1949 chini ya Mao Zedong. Walipiga marufuku matumizi ya lugha za kigeni kwenye nchi yao. Waliamua kutumia lugha yao kwenye nyanja zote, na leo kila mmoja wetu ni shahidi wa uamuzi wao ulikowafikisha.

Kwa ufupi ni kwamba, ile lugha unayoitumia uotapo ndoto- ndio lugha iwezayo kuleta mabadiliko katika maisha yako. Je, huwa unaota ndoto kwa Kiswahili au Kiingereza?
Sijakataa nafasi ya Kiswahili, lakini ukweli mchungu ni kuwa kiingereza kitaendelea kuwa muhimu zaidi, kwa mustakabali wa maendeleo yoyote ya kidunia.
 
Back
Top Bottom