Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Jana Mh Museveni na mwenyeji wake Mh Uhuru walifanya mkutano katika hoteli ya Sarova White Sand Hotel mjini Mombasa na kujadili mambo mbalimbali hasa kudumisha na kukomaza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.
Katika mkutano wao Rais Museveni alikiri kwamba sekta binafsi ndiyo nguzo kuu katika maendeleo ya nchi, na kazi kuu ya serikali ni kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Rais Museveni alisema serikali yake kwa sasa inajikita katika kupunguza gharama za kufanya biashara kwa kuhakikisha kuna upatikanaji wa umeme wa uhakika, kutengeneza na kuboresha miundombinu kama barabara na reli, pia kuhakikisha benki ya maendeleo ya Uganda (UDB) ina mtaji wa kutosha ili wafanyabiashara waweze kukopa kwa riba ndogo.
Rais Museveni akaendelea kusema kwamba ili kuhakikisha kuna maendeleo ni lazima nchi ipanue wigo wa kibiashara mpaka nje ya nchi kwani kwa kutegemea soko la ndani tuu halitatosheleza. Kwa sababu hiyo ndio maana wanasisitiza sana kuongeza ushirikiano zaidi wa nchi za Afrika Mashariki, COMESA pamoja na Continental Free Trade Area.
Rais Museveni ameishukuru serikali ya Kenya hasahasa Rais Uhuru kwa kuwezesha bidhaa za Uganda zinazopitia bandari ya Mombasa zinachukua muda mfupi kuliko kipindi cha nyuma.
Pia Rais Museveni ameishukuru serikali ya Kenya kwa kuendelea kuonesha ushirikiano wa kibiashara, baada ya mradi wa SGR na sasa wamekubali kuwapa nafasi ya kujenga bandari ya nchi kavu mjini Naivasha.
Rais Museveni pia amesema watatumia bomba la mafuta la Kisumu kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za petroli kupitia ziwa Victoria kuliko barabara ambazo huharibika haraka kutokana na uzito wa magari.