Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nchini Saudi Arabia, imeanza kuleta matunda. Waziri Ulega ameeleza kuwa kufuatia ziara hiyo, mamia ya wawekezaji Saudi Arabia wameonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika sekta ya mifugo na uvuvi nchini.
Akizungumza baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira, Maji na Kilimo wa Saudi Arabia jana, Mhandisi Abdulrahman Bin Abdulmohsen Alfadley alisema wanaangalia namna bora kwa nchi hizo mbili kushirikiana.
Alisema Saudi Arabia imevutiwa na fursa. lukuki zilizopo nchini, hususan katika sekta ya mifugo ambapo Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na maeneo mazuri ya uwekezaji.
"Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya mifugo, tunatamani kuona Saudi Arabia inafanya uwekezaji mkubwa katika eneo la malisho ya mifugo, biashara ya nyama na ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba," alisema.