Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya China ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi amesema, ziara ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini China itaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Profesa Moshi amesema, ziara ya rais Samia nchini China si kama tu ni mwanzo mpya wa uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, bali pia ni dalili ya kuimarika zaidi kwa uhusiano huo.
Aidha, Profesa Moshi ametoa mapendekezo kuhusu ushirikiano wa Tanzania na China katika ukarabati wa kisasa wa Reli ya TAZARA, na mradi wa “Daraja la Mama Samia”, na kusema anaamini kuwa kutokana na juhudi za pamoja za Tanzania na China, uhusiano wao wa kirafiki utakuwa na kiwango cha juu zaidi.
Profesa Moshi pia amepongeza mafanikio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kusema rais Xi Jinping wa China ameendelea kujitahidi kwa ajili ya ustawi wa China na dunia nzima.