Ziara ya Rose Tweve Mbunge Viti Maalum mkoa wa Iringa

Ziara ya Rose Tweve Mbunge Viti Maalum mkoa wa Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rose Tweve ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Mufindi, Kata ya Saohill ambapo ameshiriki kikao cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Upendo, Mufindi.

Ziara hiyo ni muendelezo wa kazi za Mbunge Tweve maeneo mbalimbali Mkoa wa Iringa kukagua shughuli za maendeleo na mikopo iliyotolewa kwenye vikundi vya wanawake.

Tweve amesema, Mwaka 2025 Rais ni Samia na wanawake wote wa Mufindi waendelee kuyasemea mema ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyafanya Mufindi, Saohill.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Saohill Wilaya ya Mufindi, Ndugu Rebecca Laurent Mwambusi amefurahishwa na utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Shule ya Kata ya Saohill.

Ndugu Rebecca amesema, Rais Samia Suluhu Hassan amemtua ndoo kichwani mwanamke wa Kata ya Saohill kwani kwa sasa maji ni burudani katika Kata ya Saohill.

Ndugu Rebecca amesema kwa sasa Mbole inapatikana kwa bei nafuu, Elimu imeboreshwa katika Kata ya Saohill na Wilaya nzima ya Mufindi.

Ndugu Rebecca amesema wanawake wa Kata ya Saohill wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na kuahidi kuwa mwaka 2025 watu wote wa Kata ya Saohill na Wana Mufindi wote kura za ushindi ni kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

WhatsApp Image 2023-02-24 at 23.23.47.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-24 at 23.23.46.jpeg


UWT Jeshi Imara
#KaziIendelee
 
.....Mbunge viti maalum maana yake ni nini?,huyu anawajibika kwa nani?,hili jimbo Lina so called mbunge aliyechaguliwa na wapiga kura wake na mbunge wake anawajibika kwao, sasa mbunge maalum wa nini?,huu ni ufisadi at its best, Urais wangu wa 24hrs kufikia 12clock, hawa MPs wa kimichongo watakua hawana nafasi ndani ya Bunge, Bunge ni kwa wawakilishi waliopigiwa kura na wapiga kura tu, so sad serikali yangu ni kubwa mno ndio maana gharama za uendeshaji ni kubwa mno, rudisha mkoa wa Iringa kama ulivyokua awamu ya kwanza, wananchi wanahitaji service delivers sio utitiri wa viongozi
 
Back
Top Bottom