Ziara ya Samia Moscow yatangazwa zaidi na vyombo vya habari vya nje kuliko vya Tanzania

Ziara ya Samia Moscow yatangazwa zaidi na vyombo vya habari vya nje kuliko vya Tanzania

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Ziara hii inosemwa ni ya kihistoria imekosa uhamasishaji ule unotakiwa na hii ni kutokana na vyombo vya habari vya Tanzania kuwa vimezibwa midomo na kalamu zao zimo makabatini.

Lakini vyombo vya habari vya nje vyaelezea ziara hii kwamba ni ziara ilogubikwa na ukungu wa kulegalega kwa mahusiano kati ya serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na Bunge la Ulaya.

Hata BBC nao kupitia Sammy Awami hawajaelezea vya kutosha kuhusu ziara hiyo na hiyo labda kutokana na vizuizi vilowekwa kwa upatikanaji wa taarifa zaidi.

Pia mahusiano na Marekani yamezorota kwa kiasi fulani baada ya serikali ya Marekani mapema mwaka huu kuanza kupitia upya mahusiano yake na serikali ya Tanzania.

Hiyo pia imefuatiwa na serikali hiyohiyo ua Marekani kuanza kuchukua hatua kwa kumuwekea vikwazo vya kusafiri ACP Faustine Mafwele kwenda nchini.

Kamishna huyo hatoweza kupatiwa viza ya kwenda Marekani pale atapofanya maombi na malengo halisi ya kuanza na Mafwele hayajajulikana ingawa taarifa zisizothibitishwa zadai kuwa hatua hiyo ni mojawapo ya hatua kadhaa zilizopo mezani na hatua zaidi huenda zikafuata.

Pia bunge la Ulaya lipo kwenye mchakato wa kutaka kuwepo usimamizi wa kina na masharti magumu katika msaada wake wa fedha za miradi ya maendeleo kwa serikali ya Tanzania., hadi pale itapojiridhisha kwamba serikali ya Tanzania yawajibika ipasavyo katika suala sina la kuheshimu haki za binadamu.

Tukirudi kwenye ziara ya kiserikali mjini Moscow ni kwamba kwa mujibu wa raisi Putin, Samia Hassan alipoapishwa kuwa raisi baadae alimwomba raisi Putin kufanya ziara nchini humo.

Hiyo yanaanisha kwamba ziara hii imekuwa ikiandaliwa zaidi ya miezi saba, jambo ambalo ni la kawaida kwa taratibu hizi za ziara maana kunakuwa na matayarisho ya aina zote.

Ziara hii imelenga kutoa fursa kwa delta ya utalii ambapo raia wengi wa Russia wataweza kutembelea Tanzania kufanya utalii hivyo kuweza kuingiza fedha zaidi kwenye uchumi ambao hadi sasa umedorora ingawa serikali haiko wazi kwenye hilo.

Hili la utalii litasababisha pia Tanzania kuanza kupeleka ndege yake mjini Moscow kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Kuna maeneo mengine biashara, madini na usalama ambalo halisemwi wazi lakini si jambo baya kulisema.

Hata ikisemwa kwamba mkurugenzi wa usalama yuko Moscow kupata mbinu mpya za kiusalama na kuomba msaada zaidi wa African Corps (zamani Wagner Group), si jambo la kuficha kwani yajulikana serikali imo katika kujilinda zaidi na vitisho mbalimbali ili kuendelea kukaa madarakani.

Hata Donald Trump alipofanya ziara nchini China, ilikuwa ni ziara wazi ya kibiashara na ilolenga kutafuta fursa kwa wafanyabiashara wa kimarekani nchini humo. Na kwenye msafara huo akawemo Elon Musk na matajiri wenzie kama mwenye kampuni ya Nvidia.

Jambo la msingi ambalo serikali ya Tanzania lapaswa kulitambua ni kwamba kila hatua inochukua macho ya wakubwa yapo yakiangalia. Pia macho wa wadadisi nayo yamo yakiangalia na kuchambua.

Hata TAARIFA ya wizara ya mambo ya nje ilotolewa jana kuhusu kujibu habari za Bunge la Ulaya kujadili kusitisha misaada, haikutoa ufafanuzi unoeleweka zaidi ya kile kinoonekana kujaribu kufanya “spinning”.

Hivyo hapa ndipo nafasi ya vyombo vya habari vya Tanzania vinapotakiwa kushirikishwa kwa baadhi ya waandishi kupewa nafasi ya kuambatana na msafara na pia kupewa semina ya namna ya kuitangaza ziara hiyo na pia kuelezea kwa kina faida za ziara hiyo kwa watanganyika kama nilivyoelezea hapo juu kwenye sekta ya Utalii.

Vyombo vya habari vya Tanzania vimefubaa mno viper uhuru wa kuandika bila msimamizi.
 
Ila hapa JamiiForums ziara hii imechambuliwa kwa upana na marefu , ambao vyombo vya content creators vilivyofadhiliwa na mteuliwa wa Samia anayesimamia media Paul Makonda vinaogopa.
 
Screenshot_20260604-133242~2.png
 
04 June 2026

Ruto's kSH 30M Private Jet Trip Faces Backlash After Suluhu Flies National Carrier to Russia

View: https://m.youtube.com/watch?v=Yk1ujX6dUfg
On the exact same days — June 3 to 5, 2026 — two African presidents left their countries for major state visits. Tanzania's Samia Suluhu Hassan boarded a national carrier Boeing 787 Dreamliner and flew to Moscow to meet Vladimir Putin.

Kenya's William Ruto boarded a chartered Gulfstream G550 luxury jet — master bedroom, private shower, conference lounge — and flew four hours south to Johannesburg. One president flew the flag. The other flew in style.

Meanwhile, Kenya's own presidential aircraft — Harambee One — sits grounded in a Dutch hangar, ageing, broken, and forgotten.

In this video we break down every detail: the aircraft, the costs, the Tanzania comparison that has broken the internet, the grounded Harambee One, and what all of it means for the man who built his entire presidency on the hustler promise. This is not just a story about a plane. It is a story about a broken covenant.

00:00 — Hook: Two Presidents, Two Planes, One Damning Contrast
00:42 — What Ruto Went to Do in South Africa
01:25 — The Plane: Inside the Flying Palace
02:30 — Harambee One: Rotting in the Netherlands
03:25 — Meanwhile in Moscow: What Samia Did Differently
04:20 — What Did This Trip Actually Cost You?
05:00 — Why Not Kenya Airways? The Real Answer
05:30 — The Hustler Covenant: Broken at 40,000 Feet
05:50 — Final Verdict

Sharp
 
Kurusha hilo dude la 787 inaweza kuwa pesa mkasi kuliko hata kukodi private jet!!
 
Back
Top Bottom