Ziara ya Samia nchini Urusi inakwenda kutukosesha fursa nyingi za maendeleo kutoka nchi za Magharibi

Ziara ya Samia nchini Urusi inakwenda kutukosesha fursa nyingi za maendeleo kutoka nchi za Magharibi

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Tunaenda kupoteza marafiki na washirika wa maana wa maendeleo, (US na nchi za EU) kwa tamaa ya madaraka ya watu wachache.

Inakadiriwa kuwa biashara kati ya Tanzania na Urusi ni $307m tu kwa mwaka sawa na Tsh.808b.

Tunaenda kupoteza biashara kubwa tunayofanya na nchi za Ulaya EU, inayofikia €1.2 billion sawa na Tshs 3.663 trillion kwa mwaka kupitia bajeti, afya, elimu, na maji.

Mahusiano baina ya Marekani (U.S. bilateral relations) yanatoa wastani wa $2.8 bilioni kwa mwaka sawa na Tshs 7.5 trillion kupitia uwekezaji, misaada ya maendeleo na ufadhili wa afya na elimu.

HJ_ICu9WUAEaGhP.jpeg

Tunaenda kupoteza frusa ya mikopo na misaada mingi kwenye miradi ya Maji, kilimo, barabara, reli, shule/vyuo.

Watoto wetu wengi wanasoma US na nchi za EU wachache sana wako Urusi, scholarships nyingi, research nyingi tunafanya na vyuo vya US na EU, biashara nyingi na investment kubwa, pesa nyingi tumewekeza Ulaya.

Miradi mingi mikubwa inaenda kusimamia kama sio kufa kwa kukimbilia ushirika na Urusi.

Imeelezewa kuwa kwenye ziara hii masharti makubwa ya Urusi kwa Tanzania ni kupewa miradi ya madini hasa Uranium.

Tujiulize, tangu Mrusi atusaidie kwenye vita ya Kagera almost 40 years, ni kipi kingine tangible alichotusaidia kiuchumi na kijamii, anataka kutumia matatizo yetu ya Oktoba 29 kufanya unyang'anyi wa rasilimali zetu kupitia viongozi wenye tamaa.
 
Tunaenda kupoteza marafiki na washirika wa maana wa maendeleo, (US na nchi za EU) kwa tamaa ya madaraka ya watu wachache.

Inakadiriwa kuwa biashara kati ya Tanzania na Urusi ni $307m tu kwa mwaka sawa na Tsh.808b.

Tunaenda kupoteza biashara kubwa tunayofanya na nchi za Ulaya EU, inayofikia €1.2 billion sawa na Tshs 3.663 trillion kwa mwaka kupitia bajeti, afya, elimu, na maji.

Mahusiano baina ya Marekani (U.S. bilateral relations) yanatoa wastani wa $2.8 bilioni kwa mwaka sawa na Tshs 7.5 trillion kupitia uwekezaji, misaada ya maendeleo na ufadhili wa afya na elimu.

Tunaenda kupoteza frusa ya mikopo na misaada mingi kwenye miradi ya Maji, kilimo, barabara, reli, shule/vyuo.

Miradi mingi mikubwa inaenda kusimamia kama sio kufa kwa kukimbilia ushirika na Urusi.

Imeelezewa kuwa kwenye ziara hii masharti makubwa ya Urusi kwa Tanzania ni kupewa miradi ya madini hasa Uranium.

Tujiulize, tangu Mrusi atusaidie kwenye vita ya Kagera almost 40 years, ni kipi kingine tangible alichotusaidia.
Hatufungamani na upande wowote.
Ingekuwa ni binadamu basi tungesema "tuna jinsia mbili
 
Kama hujui Historia; Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Urusi tangia miaka ya 1970. Kuna wasomi wengi tu wakiwemo madactari bingwa wamesoma Urusi. Nafikiri aombe pia kupatiwa scholarships za masomo ya Sayansi..fursa ambayo miaka ya nyuma ilikuwepo na ilitusaidia sana kupata madactari Bingwa.

Sisi hatuendi Urusi kuunga mkono vita yake na Ukraine au pengine Kuisaidia Urusi? ILE NI FRIENDLY VISIT!.
Kitendo cha kufikiri kuwa, hata Nchi ya kuitembelea inabidi upangiwe na wakoloni; ni ukosefu wa maarifa au niseme; ni utumwa wa kifkra

Tanzania hatufungamani na upande wowote
 
Hii kama mkomesheni MAREKANI

Ni hivi alishadadia sana machafuko na kukosoa uchaguzi wa 2025.. so kana kwamba ameamua kuwa nusu adui na uongozi wa tanzania hauna hiyana
Umeona ujisogeze urusi zaidi

Kwani siku hizi hakuna kumuogopa mtu ukiwawekea watu vikwazo wanaangalia njia nyingine
 
.... mbona hata viongozi wa Marekani na nchi zingine za magharibi wanawasiliana, kutembelea na kufanya biashara na Urrusi? ... Mama Samia kafanya lipi jipya?
TUJITEGEMEE!
Wale ni big fish wanajuana usilinganishe na dagaa kama sisi utaumia, pamoja na tofauti zao juzi Trump alikuwa China.
 
Kama hujui Historia, Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Urusi tangia miaka ya 1970. Kuna wasomi wengi tu wakiwemo madactari bingwa wamesoma Urusi. Nafikiri aombe pia kupatiwa scholarships za masomo ya Sayansi..fursa ambayo miaka ya nyuma ilikuwepo na ilitusaidia sana kupata madactari Bingwa.
Sisi hatuendi Urusi kuunga mkono vita yake na Ukraine au pengine Kuisaidia Urusi? ILE NI FRIENDLY VISIT!.
Kitendo cha kufikiri kuwa, hata Nchi ya kuitembelea inabidi upangiwe na wakoloni; ni ukosefu wa maarifa au niseme; ni utumwa wa kifkra!!!
TANZANIA HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE!!!
Ile siyo friend visit ni business visit.

Ndio maana nimeuliza tangu miaka ile ya 70 na 80 ni kipi kwa miaka ya hivi karibuni alichotusaidia.
 
Wale ni big fish wanajuana usilinganishe na dagaa kama sisi utaumia, pamoja na matatizo yao juzi Trump alikuwa China.
... Trump alipokuwa China alikuwa anaiwakilisha na Tanzania? ... au unataka kusema sisi tukitaka kwenda China au Russia lazima tupate kibali Marekani? TOKA LINI TZ NI JIMBO LA MAREKANI?

Unaleta mihemuko, jadili faida na hasara ya ziara badala ya nani anatupangia kwenda wapi.

Leo unaweza kwenda Iran hukatazwi lkn kabla ya kwenda Iran angalia faida na hasara yake.
 
Ile siyo friend visit ni business visit.

Ndio maana nimeuliza tangu miaka ile ya 70 na 80 ni kipi kwa miaka ya hivi karibuni alichotusaidia.
Kwanini akili inawaza kusaidiwa saidiwa tu?
Sisi kama taifa tutaanza lini kuwaza kujitegemea?
 
Back
Top Bottom