Hatufungamani na upande wowote.Tunaenda kupoteza marafiki na washirika wa maana wa maendeleo, (US na nchi za EU) kwa tamaa ya madaraka ya watu wachache.
Inakadiriwa kuwa biashara kati ya Tanzania na Urusi ni $307m tu kwa mwaka sawa na Tsh.808b.
Tunaenda kupoteza biashara kubwa tunayofanya na nchi za Ulaya EU, inayofikia €1.2 billion sawa na Tshs 3.663 trillion kwa mwaka kupitia bajeti, afya, elimu, na maji.
Mahusiano baina ya Marekani (U.S. bilateral relations) yanatoa wastani wa $2.8 bilioni kwa mwaka sawa na Tshs 7.5 trillion kupitia uwekezaji, misaada ya maendeleo na ufadhili wa afya na elimu.
Tunaenda kupoteza frusa ya mikopo na misaada mingi kwenye miradi ya Maji, kilimo, barabara, reli, shule/vyuo.
Miradi mingi mikubwa inaenda kusimamia kama sio kufa kwa kukimbilia ushirika na Urusi.
Imeelezewa kuwa kwenye ziara hii masharti makubwa ya Urusi kwa Tanzania ni kupewa miradi ya madini hasa Uranium.
Tujiulize, tangu Mrusi atusaidie kwenye vita ya Kagera almost 40 years, ni kipi kingine tangible alichotusaidia.
Wale ni big fish wanajuana usilinganishe na dagaa kama sisi utaumia, pamoja na tofauti zao juzi Trump alikuwa China..... mbona hata viongozi wa Marekani na nchi zingine za magharibi wanawasiliana, kutembelea na kufanya biashara na Urrusi? ... Mama Samia kafanya lipi jipya?
TUJITEGEMEE!
Ile siyo friend visit ni business visit.Kama hujui Historia, Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Urusi tangia miaka ya 1970. Kuna wasomi wengi tu wakiwemo madactari bingwa wamesoma Urusi. Nafikiri aombe pia kupatiwa scholarships za masomo ya Sayansi..fursa ambayo miaka ya nyuma ilikuwepo na ilitusaidia sana kupata madactari Bingwa.
Sisi hatuendi Urusi kuunga mkono vita yake na Ukraine au pengine Kuisaidia Urusi? ILE NI FRIENDLY VISIT!.
Kitendo cha kufikiri kuwa, hata Nchi ya kuitembelea inabidi upangiwe na wakoloni; ni ukosefu wa maarifa au niseme; ni utumwa wa kifkra!!!
TANZANIA HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE!!!
... Trump alipokuwa China alikuwa anaiwakilisha na Tanzania? ... au unataka kusema sisi tukitaka kwenda China au Russia lazima tupate kibali Marekani? TOKA LINI TZ NI JIMBO LA MAREKANI?Wale ni big fish wanajuana usilinganishe na dagaa kama sisi utaumia, pamoja na matatizo yao juzi Trump alikuwa China.
Unaleta mihemuko, jadili faida na hasara ya ziara badala ya nani anatupangia kwenda wapi.... Trump alipokuwa China alikuwa anaiwakilisha na Tanzania? ... au unataka kusema sisi tukitaka kwenda China au Russia lazima tupate kibali Marekani? TOKA LINI TZ NI JIMBO LA MAREKANI?
TUJITEGEMEE!
Tatizo lako unawaza ki chawa chawa, yaani kikubwa tumbo lako lishibe!... Trump alipokuwa China alikuwa anaiwakilisha na Tanzania? ... au unataka kusema sisi tukitaka kwenda China au Russia lazima tupate kibali Marekani? TOKA LINI TZ NI JIMBO LA MAREKANI?
TUJITEGEMEE!
Kujitegemea ndio kitu hatukitaki, tumeshazoea misaada kiasi cha kuhisi tupo duniani kupokea misaada ya wazungu..... mbona hata viongozi wa Marekani na nchi zingine za magharibi wanawasiliana, kutembelea na kufanya biashara na Urrusi? ... Mama Samia kafanya lipi jipya?
TUJITEGEMEE!
Hapa ulitakiwa kutetea hoja yako, ila kwa kuwa huna maelezo ya msingi unaishi kuleta vihoja.Tatizo lako unawaza ki chawa chawa, yaani kikubwa tumbo lako lishibe!
Kwani nani kakwambia inafungama.Tanzania haifungamani na upande wowote
Sasa kwenda urusi ni kosa?Kwani nani kakwambia inafungama.
Kwanini akili inawaza kusaidiwa saidiwa tu?Ile siyo friend visit ni business visit.
Ndio maana nimeuliza tangu miaka ile ya 70 na 80 ni kipi kwa miaka ya hivi karibuni alichotusaidia.