Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
🛑ZIARA YA UVCCM SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC)
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakiongoza Mwenyekiti Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) wamefika kituo Cha reli ya kisasa (SGR) cha Dar es salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa.
Lengo la ziara hio ni kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwenye mradi huo na kupata elimu ya namna Shirika la Reli Tanzania (TRC) linajiendesha mara baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ziara hii inahusisha Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Wenyeviti wa Mikoa yote nchini na Makatibu wa UVCCM Mikoa yote.
#Kaziinaendelea
Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.