Mjopho
Member
- Aug 21, 2025
- 78
- 149
Ikiwa ni mwanzo kabisa wa msimu mpya wa mashindani mbalimbali ya soka ulimwengu, na baadhi ya mashindano makubwa na maarufu ya mchezo wa soka yakiwa tayari yameisha anza kutimua vumbi rasmi na mengine yakiwa mbioni kuanza katika siku chache zijazo. Sio vibaya kwa muda huu kufahamishana na kukumbushana baadhi ya timu zilizowahi kufanya comeback 'kupindua meza' na kushangaza wapenzi wengi wa mchezo wa soka.
1. Liverpool 3–3 AC Milan (2005 UEFA Champions League Final) ###The Miracle of Istanbul
Hii ilikuwa mechi ya fainali ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka 2005 ikihusisha timu za Liverpool dhidi ya wababe kutoka Italy AC Milan. Unajua nini mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Liverpool walikuwa nyuma kwa jumla ya mabao matatu kwa bila, ila baada ya kipenga cha kuashiria kuanza kipindi cha pili kupulizwa mambo yalibadilika na Liverpool walipata mabao matatu ndani ya dakika 6 tu mabao ambayo yalifungwa na Legend Steven Gerrard dakika ya 54, Šmicer dakika ya 56 pamoja na Xabi Alonso mnamo dakika ya 60. Jambo ambalo lilifanya mechi kuisha kwa sare ya mabao matatu kwa matatu na Liverpool kuchukua ubingwa kwa ushindi wa mikwaju ya penati tatu kwa mbili.
2. Ajax 2-3 Tottenham (2019 UEFA Champions League Semi-Final) Date: May 8, 2019
Hakuna mtu alietarajia baada ya Spurs kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza wakiwa nyumbani kwa bao moja bila, Mechi ya mkondo wa pili wakiwa ugenini bila ya nyota wao mahiri Harry Kane tena dhidi ya Ajax ambao wako moto wakiwa tayari wamezitoa timu kongwe real madrid pamoja na Juventus ya cristiano ronaldo. Hadi kipindi cha kwanza kinatamatika wenyeji walikuwa mbele kwa magolo mawili na kufanya kuongoza kwa jumla ya mabao matatu kwa bila. Kama wasemavyo waswahili mtu sie nyau kipindi cha pili kilianza huku ulimwengu ukishuhudia maajabu toka kwa kijana Lucas moura aliefunga magoli matatu na kufanya mechi kutamatika kwa ushindi wa mabao matatu kwa mawili na Spurs wakitinga fainali kwa ushindi wa bao la ugenini.
3. Newcastle United 4–4 Arsenal (2011 Premier League)
Turudi pale kwenye ardhi ya malkia tuwaangazie wabeba mitutu wa jiji la London ambapo mnamo Sat 05 Fe 2011 ilikuwa katika Matchweek 26 wakiwa wamewatembelea Newcastle United, Ndugu zetu mpaka kipindi cha kwanza kinatamatika walikuwa wanaongoza bao nne bila, ila kilichotokea kipindi cha pili ni maajabu ya mussa na firauni ambapo wenyeji walifanikiwa kupata mabao manne na kufanya mchezo kutamatika kwa sare.
4. Manchester City 3–2 Aston Villa (2022 Premier League)
Unakumbuka mechi hii?, siku ambayo Manchester city walikuwa wanahijati ushindi ili wanyakue ubingwa watu walibaki midomo wazi maana hadi kufikia dakika ya 75 City walikuwa nyuma kwa jumla ya mabao mawili kwa bila, huku matumaini yakiwa upande wa mashibiki wa Liverppol kuwa wanakaribia kutwaa ubingwa kilichotokea baada ya hapo ilibaki stori ndani ya dakika chache matokea yalibadilika na ubao kusoma City tatu na Aston Villa mbili, shukran kwa magoli ya
Gundogan dakika ya 76' na 81' huku goli lingine likifungwa na Rodri.
5. Manchester City F.C. 3–2 Queens Park Rangers F.C.
Hii ilikuwa mechi ya matukio ikiwa mahasimu wa upande wa pili wa jiji la Manchester yaani Manchester united wakiwa tayari mechi yao imetamatika kwa ushindi wakisubiri kumalizika kwa mechi hii ili watangazwe mabingwa wa Uingereza, tayari washaanza maandalizi ya sherehe za ubingwa, vijana wa Manchestrer city chini ya kocha Mancini walisikika wakisema 'hold my beer' na kuanza safari ya kusimika utawala wao pale uingereza baada ya goli la kusawazisha toka kwa Edin Dzeko na kufuitiwa na golo la ushindi la dakika za jiooooni kutoka kwaa mwamba Sergio kun Aguuero na kuwapa Manchestrer city ubingwa baada ya miaka mingi kupita .
Wewe mdau unakumbuka Comeback ipi? na ulikwa wapi? na uliyapokeaje matokeo hayo?