Kuhusu oil.. jamaa wadau wameelezea vizuri, nami niweke kamchango kangu kidogo.
Mineral oil ambazo ni non synthetic oil zina changamoto ya kutengeneza carbon kwenye injini kama zisipo badilishwa kwa wakati
Synthetic oil kwakua zina additives zinazofanya ziweze kumantain viscosity yake hata zikiwa exposed to high temperature for extended time... Lakini si kusubiri mpaka gari ifikishe km 10,000 ndo ubadili oil.. utaua injini yako.
Ubora wa oil.. ubora wa oil una angalia urahisi wa oil ku flow wakati wa low temperature na uwezo wa ku-maintain thickness ya oil wakati wa high temperature, carbon formation kwenye engine, evaporation rate ya oil.
Matumizi ya oil kwenye Gari.. oil ufanya kazi ya lubrication kwenye moving parts, sasa hizi moving parts ndan ya injini huwa zinakua na certain clearance kwa ajili ya oil kukaa ili kuzuia physical contact between moving parts.. hapa sasa ndo bongo kuna shida. Unakuta manufacturer kaandika gari yake inatumia oil 5w-30.. hapa mzungu kaisha jua kwamba kwa clearance iliyopo kwenye components za injini basi oil ya viscosity fulan itafaa, sasa mbongo anaenda chukua oil nzito Kama sae 40 au 20w-50 anatia ndani ya gari.. sasa kumbe hapa anatengeneza tatizo. Hizi oil ni zito sana zinaongeza pressure kwenye moving parts kwakua clearance inakua ni ndogo ulinganisha na thickness ya oil hasa during cold start.. mpaka baadae oil ikisha pungua thickness because of temperature. Sasa gari nyingi hapa Tanzania hufa kwasababu ya oil hizi nzito hasa wakati wa asubuh ambapo kwakua hizi oil ni nzito, ukiwasha Gari for the first time oil inachelewa kupanda juu kwenye cam shafts, vvti system na kufika kwenye cylinder wall kwakua oil ni nene na hai flow kwa wakati.. sasa unakuta hadi injini inatoa sauti za ajabu wakati inapowaka for the first time, then zile sauti zinapotea baada ya oil kufika kwenye yale maeneo kwakua tayari injini imechemka na oil imelainika.. na situation huwa mbaya zaidi kama umetoa thermostat kwakua injini inachelewa ku attain required temperature so na oil inashidwa yeyuka kwa wakati, na kama kukiwa na extended usage ya hizi thick oil wakati mwingine huua (destroy) rings za oil kwenye piston kwakua oil inashindwa kupita kwenye vitundu vya piston kurudisha oil kwenye sump.. nakuleta tatizo gari kula oil.. lakini pia kuua piston rings because of excessive compression inayosababishwa na thick oil na kuleta shida pia ya injini kula oil in long run.
Kuhusu interval ya ku change oil.. watu wengi sisi tuna angalia kilometers tu peke yake Gari imetembea ili kubadili oil, ila tuna sahau kuna muda Gari ina unguruma hata saa nzima bila kwenda popote ila oil inaungua.. sasa hapa kama una angalia tu km shauri yako utaua injini mapema.. ni vizuri kuangalia oil ipo kwenye hali gani hasa kama gari ina kaa sana kwenye folen injini ikiwa on.
Pia kama ni mtu unatembea short distance unazima gari mara unawasha zima kila wakati.. hii pia hufanya oil iwe contaminated na gasoline.. kumbuka gari inapowaka injekta (fuel injectors) humwaga mafuta mengi ila kufanya gari iwake, so sio mafuta yote huungua, mengine hupenya na kwenda kwenye sump ya oil, so haya yanayopenya huenda ku contaminate oil na kuifanya oil ipungue ubora wake with time.
Pia kama unasafiri zaid ya miezi sita na gar ikakaa 6months bila kuwaka hata kama uliondoka umeweka oil mpya ukija toa hiyo oil weka nyingine.
Interval ya oil changing.. kama watumia mineral oil kwa mazingira yetu ya kitropic na hizi folen za mjini change oil from 2500km to 3000km.. na hakikisha watumia quality oil zisizokua na rate kubwa ya utengenezaji wa carbon au rate kubwa ya oxidation.
Kwa wa synthetic oil change after every 5000km na sio kwenda mpaka km7000-10,000 hata kama watumia liquimo oil. (Na hapa lazima uwe na uhakika gari yako haina tatizo la kula oil. Kama inakula oil utakuta unaweka hizi kwakua ni nyepesi mpaka unafika km 5000 unakuta umebakiwa na oil lita moja)
Kuhusiana na quality ya oil, tafuta oil zenye API rating nzuri hasa ukiwa na gari zenye GDI fuel system au pia ukiwa na Gari ya Turbo.
Kuhusiana na oil za gearbox (transmission fluid) weka recommended transmission fluid ambazo manufacturer wako ame recommend.. kama ni ATF-TYPE 4, CVT-TC, or CVT-FE, WS, NS-2 or3, Matic J, DSG nk.. ili mradi ni recommended.. and avoid universal transmission fluids.. na transmission hubadilishwa after at least every 30,000km but you can go more than that depending na mazingira gari inatumika..