SoC02 Zifahamu haki zako kama mfanyakazi

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 2, 2022
Posts
60
Reaction score
75
1. Utangulizi

Idadi kubwa ya wafanyakazi Tanzania hawazifahamu haki zao jambo ambalo linapelekea kunyonywa, kukandamizwa, kunyanyaswa, na kudhalilishwa na waajiri wao kwa njia mbalimbali kama kulipwa ujira mdogo, kufanya kazi katika mazingira ambayo si salama kwa afya zao, kukosa ulinzi wa ajira, unyanyasaji wa kijinisa mfano wanawake wengi na wanaume baadhi wanakumbwa na unyasaji wa kijinsia kutoka kwa waajiri wao. Hivyobasi lengo langu kuu ni kumfahamisha mfanyakazi haki zake anapokuwa katika mazingira ya kazi.

2. Mfanyakazi ni nani?

Mfanyakazi; Mtu yeyote aliyeingia katika mkataba wa ajira wa aina yoyote kumfanyia kazi mtu mwingine kwa ujira (Malipo). Mfanyakazi anaweza kuwa wa mfanyakazi wa muda mrefu, mfanyakazi wa muda mfupi, mfanyakazi wa kazi maalum, na mfanyakazi wa msimu, hiyo ni kulingana na makubaliano ya makataba walioingia kati ya mfanyakazi na mwajiri wake.

3. Haki za mfanyakazi ni zipi?

Haki za mfanyakazi ni haki ambazo zipo zinatambulika kisheria na haki za binadamu zinazohusiana na mahusiano ya kazi kati ya wafanyakazi na waajiri. Haki hizi zimeratibiwa katika sheria ya kitaifa na kimataifa ya kazi na ajira. Kwa mfano kwa Tanzania tuna sheria mbalimbali kama Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6 ya 2004, Sheria ya Taasisi za Kazi Namba 7 ya 2004, Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ya 2008, na Sheria ya Kazi na Afya ya 2003. ambazo nimeelezea haki za mfanyakazi anapokuwa katika eneo la kazi.

3.1. Haki ya kufanya kazi katika mazingira ambayo ni salama kwa afya.

Mfanyakazi anahaki ya kukingwa na hatari mbalimbali zinaweza kuathiri usalama na afya zao wakiwa katika maeneo ya kazi. Kwamfano kuvaa vifaa vya kujikinga na hatari mbalimbali husisani pale mfanyakazi anapofanya kazi maeneo yenye hatari au anapofanya kazi zinazoweza kuathiri afya na usalama wake Pia mfanyakazi anahaki ya kupewa mafunzo kuhusiana na usalama na afya wake pindi anapokuwa maeneo ya kazi. Sura ya 95 ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa kazi, 2003 inamtaka Mwajiri kutoa mazingira yenye afya na salama kwa wafanyakazi na kufidia wafanyakazi walioathirika kiafya kutokana na mazingira ya kazi.

3.2. Haki ya uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi

Mfanyakazi anahaki ya kuwa na uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi ( Trade Unions). Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa maelekezo juu ya uhuru wa kujumuika. Pia sehemu ya 9 ya Sheria ya kazi na Mahusiano Kazini inamruhusu mwajiri na wafanyakazi kujiunga na vyama vyao. Pia wafanyakazi wanaruhusiwa kushiriki shughuli mbalimbali za kichama nje ya masaa ya kazi. Mfanyakazi hapaswi kutengwa kwa kujihusisha kwake na shughuli za chama cha wafanyakazi ambacho yeye ni mwanachama.

3.3. Haki ya Kugoma

Haki ya mfanyakazi kugoma inatambulika kisheria ingawa haki hii inamasharti yakufuata. Kwa baadhi ya sekta za uchumi migomo hairuhusiwi, husuani sekta zinazotoa huduma muhimu kama umeme, maji, huduma za afya nk. Kabla ya mfanyakazi kufanya mgomo lazima kuwe na siku 30 za upatanishi wa pande mbili ambazo ni upande wa mwajiri na upande wa mfanyakazi baada ya kushindwa ndipo mgomo utafuata. (sehemu ya 75 hadi 85 ya sheria ya kazi na mahusiano, 2004).

3.4. Haki ya kupewa likizo

Mfanyakazi anahaki ya kupata likizo mbalimbali kama ilivyoelezwa katika sheria ya kazi na mahusiano sehemu ya 29 – 34 baadhi ya likizo hizo ni likizo ya muhula ambapo mfanyakazi anahaki ya kuchukua likizo yenye malipo ya angalau siku 28 katika kila mzinguko wa likizo, Likizo ya uzazi kwa wanawake (Martenity leave) Mfanyakazi mwanamke ana haki ya walau wiki kumi na mbili ambazo ni sabasaba na siku (84) za likizo ya uzazi na kuendelea kupata mshahara wake. Atapata walau siku 100 za likizo ya uzazi endapo amejifungua watoto zaidi ya mmoja (mapacha). Pia ana haki ya kupata siku nyingine 84 za likizo hiyo endapo mtoto wake atafariki ndani ya mwaka wake wa kuzaliwa. Likizo ya uzazi kwa mwanaume (Paternity leave) Mwanamme nae anayo haki ya mapumziko ya siku tatu (3) bila kukatwa mshahara pindi mke wake wa ndoa anapojifungua mtoto. Likizo ya ugonjwa Mfanyakazi anapokuwa mgonjwa anahaki ya kupewa likizo ya angalau siku 126 katika kila mzunguko wa likizo kama iliyotajwa katika sheria ya kazi na mahusiano italazimika kukotolewa kwasiku 63 za kwanza zitatakiwa kulipwa mshahara mzima, siku 63 zinazofuata zitatakiwa kulipwa nusu mshahara.

3.5. Haki ya kulipwa fidia

Mfanyakazi pia anahaki ya kulipwa malipo ya fidia mbalimbali, kwa mfano malipo ya masaa ya ziada ya kazi, kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya kazi na mahusiano ya mwaka 2004 sehemu ya 19. Pia mapumziko ya fidia kwa kufanya kazi siku za mapuumziko, na Fidia ya kufanya kazi siku za mapumziko ya Juma au Sikukuu za Kitaifa Iwapo mfanyakazi atafanya kazi siku za mapumziko ya juma au sikukuu za kitaifa atakuwa na haki ya kulipwa mara mbili ya mshahara wake wa siku wa kawaida. (Sehemu ya 24 na 25 ya sheria ya kazi na mahusiano kazini ya 2004) Kwa mujibu wa sehemu 7 ya sheria ya mshahara ya 2010.

3.6. Haki ya kupata Ujira

Mfanyakazi anahaki ya kupata ujira Sheria ya kazi na Mahusiano ya mwaka 2004 inaratibu malipo ya mishahara kwa kada zote za wafanyakazi. Kwa mujibu wa Sehemu ya 26 ya sheria, Ujira unaweza kukokotolewa kwa saa, siku, juma au mwezi. Sehemu ya 27 inamtaka mwajiri ulipa wafanyakazi wake ujira wao wakati wa siku ya kazi kadri walivyo kubaliana kwenye mkataba wa kazi. Kila mtu, bila ubaguzi wa aina yeyote, anahaki ya kupata ujira kutokana na kazi na wote wanaofanya kazi, wanaoaswa kupata stahiki zao za malipo kwa kadiri ya utendaji na sifa za kufanya kazi husika. Kila mtu ana haki ya kupata malipo stahiki.

3.7. Haki ya kuhakikishiwa usalama wa ajira

Mfanyakazi pia anahaki ya kuhakikishiwa usalama wa ajira kwa kupewa hati ya maandishi ya majukumu yake ya kazi anapoanza kazi Taarifa hizo ni jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi, mahali alipoajiriwa, kazi zake tarehe ya kuanza, muundo na muda wa mkataba, kituo cha kazi, masaa ya kazi, ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu na kitu kingine kilichotajwa. (Sehemu ya 15 ya sheria ya kazi na mahusiano kazini, 2004). Pia mfanyakazi anaweza kuhakikishiwa usalama wa ajira kwa kupewa mkataba wa kazi kulingana na sheria ya kazi na mahusiano kazini makataba huo unaweza kuwa mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za wataalamu na mameneja, mkataba wa kazi maalumu.

4. Hitimisho

Mfanyakazi Kuzifahamu haki zake ni muhimu sana kwa sababu itamsaidia kufanya kazi katika mazingira ambayo ni salama kwa afya zao, kufanya kazi kwa kufuata muda uliowekwa na sheria, kupewa mikataba ya ajira, kulipwa mishahara mizuri itakayowasaidia kuboresha hali zao za maisha, kuhusika katika kufanya maamuzi katika eneo la kazi, kupewa ulinzi wa kijamii kama vile bima ya afya, fidia zao wanapojeruhiwa mahali pa kazi, na kupata mafao ya kustaafu wanapostaafu, pia mazingira ya kazi yataongezeka kwa wafanyakazi kwa sababu wanajua haki zao wakiwa kazini.
 
Upvote 6

ok
 
Back
Top Bottom