Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Ndugu zangu tunapozungumzia Mataifa makubwa tunawalenga Marekani, Ujerumani, Wiingereza, Japan, China, Korea nakadhalika.
Haya ni mataifa makubwa yalifanikiwa tangu zamani na wakati mwingine mataifa mengine yanajiuliza ni mbinu gani wanazotumia kufanikiwa.
Jambo la kushangaza ni kuwa mbinu wanazotumia kufanikiwa sio nyingi ni chache sana ikiwemo kuchagua viongozi wenye akili kubwa wanaochukia ujinga.
Haya mataifa huwa hayachagui viongozi wajinga, wavivu, wenye tamaa, masikini, wanaokumbatia ufisaidi, wasio na maono ya Taifa, vichaa kwa vyovyote vile ilimradi viongozi wa hovyo.
Hivi vigezo huwa wanakuwa makini kuhakikisha kuwa hao viongozi wanaochaguliwa hawana kasoro hizo kwasababu wanafahamu madhara ya viongozi wajinga huwa wanasababisha matatizo kwa wananchi wao.
Sifa ya kwanza kabisa watatazama elimu yao ni ya kiwango gani, uerevu wao, hali yao ya kiuchumi, wanaothamini utu, ukakamavu na ndio maana viongozi ni lazima wawe wamefuzu mafunzo ya jeshi, viongozi wanaochukia ujinga, tamaa, wenye maono ya Taifa lao.
Viongozi wa Mataifa hayo makubwa wakishakuwa na vigezo hivi basi wataongoza Taifa hilo na wataleta mafanikio makubwa sana kwa Wananchi wao ndio maana tunaona Marekani, Ujerumani, Wiingereza, Japan, China wakipiga hatua kwa kiasi kikubwa.
Wananchi wa Taifa lolote wanapaswa kutambua kuwa viongozi wajinga huleta matatizo kwa wanachi wao, hivyo basi wachague viongozi werevu, wanaochukia ujinga, wenye elimu kubwa, wanaothamini utu na wenye maono kwa Taifa lao ili matatizo ya Wananchi yapungue ama kukoma kabisa.