Zifahamu nchi ambazo jua halizami

Zifahamu nchi ambazo jua halizami

Kwa sababu Alaska hupata jua kwa kipindi kirefu miezi ya may na julai hivyo mimea hujitengenezea chakula chake kwa wingi Zaidi (Photosynthesis) hivyo kupelekes mimea kua mikuuubwa kuliko kawaida hasa mimea yenye Nutrients za vitamins known as Vegetables.

Tango la kuvunja chagašŸ˜…View attachment 2373736
Hii imekaa kisayansi au nadharia tu
Maana huku kwetu jua linatuwakia miezi kibao lakn mazao hayawi kwa ukubwa huo
 
Ni tamaduni kwa kila siku Jua kuchomoza alfajiri na kuzama jioni, kisha kiza kutawala.

Lakini hii ni tofauti kwa baadhi ya nchi ambazo kwao jua kuzama ni kama maajabu kwao. Nchi hizo ni Sweden, Finland, Norway, Canada(Nunavut), Iceland na Alaska(Barrow).

Sweden, kwao huweza kukaa mpaka miezi sita kwa mwaka bila ya jua kuzama. Inapofika mwezi Mei mpaka Agosti, jua huzama usiku wa manane na kuchomoza alfajiri ya saa 10.

Finland, mara zote wakati wa majira ya joto kwa siku 73 mfululizo jua halizami kabisa lakini wakati wa baridi jua halichomozi kabisa.

Norway, kwao pia jua halizami kwa takribani siku 76 mfululizo. Lakini kuanzia mwezi Mei mpaka mwishoni mwa mwezi Julai kunakua na kuzama kwa jua lakini kwa muda mfupi sana.

Nunavut, Canada nako hukaa kwa miezi miwili mfululizo bila ya jua kuzama ila wakati wa baridi mji huo hupita siku 30 bila kupata Jua.

Iceland, ni nchi ambayo mwezi Juni wote huisha bila ya Jua kuzama haswa wakati wa majira ya joto.

Barrow, Alaska kwenye mji huu Jua halizami kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei mpaka mwishoni mwa mwezi Julai na mwanzoni mwa mwezi Novemba jua halizami pia kwa siku 30 mfululizo.
Uongo
 
Bora lisingekuwa linazama Tz tupunguze idadi ya wachawi Ili tushuke kwenye top two uchawi Africa🤣🤣🤣
 
Jua linakuwa halionekani buana inakuwa km dalili ya mvua hivi uache uongo
Hii hali kama hujaishi kwenye hizo nchi unaweza usiamini. Sema saa nyingine inakuaga ya kifala sana. Imagine saa nne usiku jua linawaka na unatakiwa kulala. Au unaenda club saa tano usiku jua linawaka huko nje. Ukitoka saa tisa usiku jua kali..

Kimbembe kinakuja kipindi cha winta. Saa nne asubuhi giza totoro hakujakucha bado, kunaanza kupambazuka saa tano tano ikifika saa nane mchana jua linazama usiku unaingia.
 
Scandinavian country's ndo ziliitwa zamani

Zilisifika kwa utajiri sijui sasa hali iko je.

Bora huku kwetu lisingezama tufanye kazi 24 hours daily [emoji1787][emoji1787]
Huku linawaka mchana lakin vijana wapo vijiweni kulaum serikali je lingewaka 24hr ingekuwaje?
 
Ingependeza kama tungepata na sababu za kijografia ili tusiishie kutikisa kichwa tuu. Wengine geography kushoto kabisa
Ni kuchange kwa mhimili wa dunia (earth's axis) kwa almost 23 degrees so kutokana shape ya dunia iliyopo kama yai (oval) husababisha polar regions kuwa titled away from the sun, yani dunia inakuwa kama imeegemea upande mmoja so hata iki rotate kuna maeneo ya polar regions hayataweza kuli face jua so hapo hawatapata jua.

Ni theory rahisi kuielewa ila lugha yetu nayo ni ngumu kuitumia kuelezea mambo ya kisayansi.
 
Back
Top Bottom