KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 675
SABABU ZA GARI YA DIESEL KUA BEI JUU KULIKO PETROL
Na Kimomwe Motors (T) Ltd- Waagizaji Magari
1. Uzito wa mafuta ya Diesel unaopelekea gari kutumia mafuta chini zaidi kwa wastani wa asilimia 15 mpaka 20 kulinganisha na gari za Petrol. Mfano, BMW X5 ya Diesel Cc 3000 inakadiriwa kwenda km 11 kwa lita wakati X5 ya Petrol Cc 3000 inakadiriwa kwenda km 8 kwa lita. hivyo watu wengi huhitaji zaidi gari za Diesel ili kupunguza gharama za mafuta
2. Uimara wa mda mrefu wa injini za Diesel. Kwa mda mrefu sana injini za Diesel zimejiwekea heshima kwa kua injini zinazodumu kwa mda mrefu ikilinganishwa na injini za petrol. Mifano ya injini zilizoweka heshima ya injini hizi kuaminika kwa kudumu ni kama 1HZ, 2L, 3L, 5L, injini zote za Landrover za Diesel, Injini zote Ford za Diesel, Injini zote za Toyota Hilux za Diesel maarufu kama D4D. n.k Hii pia inavutia uhitaji mkubwa wa gari hizo hivyo gharama lazima iwe juu kidogo
3. Ushuru wa gari za Diesel kua juu. Tukilinganisha X5 ya Petrol na Diesel, ushuru wa Diesel uko juu kwa hivyo kufanya bei iongezeke zaidi. Sababu ya ushuru kua juu ni uzalishwaji wa hewa na Nitrogen pamoja na hewa nyingine zinazoweza kuleta madhara kwa binadamu haswa changamoto ya upumuaji...pamoja na sauti ya juu inayopatikana katika gari za Diesel.
4. Historia inayoonesha kua kwa miaka mingi ya iliyopita, mafuta ya Diesel yaliuzwa kwa bei nafuu kuliko Petrol hivyo kuvutia wamiliki wengi wa magari kukimbiliza hizi za Diesel jambo lililofanya thamani ya gari hizo kua juu kutokana na uhitaji wake.
nadhani hayo machache yatatoa mwanga kwa nini gari za Diesel hua bei juu kulinganisha na zinazotumia Petrol.
Kwa msaada na Ushauri tembelea ofisi zetu za Dar na Mbeya