Zijue ABE Coated Pumpkin Seeds: Mbegu bora za Maboga Zilizookwa

Zijue ABE Coated Pumpkin Seeds: Mbegu bora za Maboga Zilizookwa

Mbepo yamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2012
Posts
1,466
Reaction score
2,285
Wanandugu leo nawaletea mbegu za maboga zilizookwa. Hizi ni mbegu zilizoandaliwa kwa mazingira bora kabisa kuahakikisha kiini kinabaki na afya yake bila kuungua huku ukila mbegu tamu kabisa. Mbegu hii ni ya kwanza na ya aina yake hapa jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani ikiwa na sukari na nazi. Utamu wake umeuzidi wa korosho na ulapo utapata hamu ya kula tena na tena.

Endelea kufuatilia uzi huu kujua faida ya mbegu za maboga kwa afya yako
 

Attachments

  • IMG-20190314-WA0017 (1).jpg
    IMG-20190314-WA0017 (1).jpg
    69.1 KB · Views: 30
Faida zitokanazo na ulaji wa mbegu za maboga zimegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo

1. Faida kwa mama mjamzito
2. Faida kwa mama anayenyonyesha
3. Faida kwa mtoto mdogo
4. Faida kwa wanawake kwa ujumla
5. Faida kwa wanaume
6. Faida kwa wazee
7. Faida kwa wote kwa ujumla wake
 
Najua baada ya maelezo mengi na kuzimwagia sifa kemkem, kwenye umaliziaji utasema unazo na unauza kwa bei nafuu, huku ukiambatanisha na namba ya simu kwa mwenye atahitaji....[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika hizo faida zake,ikikosekana faida ya nguvu za kiume basi utakua unaliua soko wewe mwenyewe.😀😀
 
Katika hizo faida zake,ikikosekana faida ya nguvu za kiume basi utakua unaliua soko wewe mwenyewe.😀😀
Hii ipo pia. Ni muhimu ila siyo hitaji la lazima ikilinganishwa na faida nyingine. Kwa asilimia kubwa sana watu wanaugua magonjwa yasiyoambukiza ambayo husababishwa na mfumo wa maisha. Ukienda mahospitali hutakuta watu wamelazwa kwa kukosa nguvu za kiume, ila magonjwa mengine ambayo mbegu hizi matumizi yake hupunguza sana hatari ya kuyapata hayo magonjwa.
 
Najua baada ya maelezo mengi na kuzimwagia sifa kemkem, kwenye umaliziaji utasema unazo na unauza kwa bei nafuu, huku ukiambatanisha na namba ya simu kwa mwenye atahitaji....[emoji23][emoji23][emoji23]
Duh! Hapana usiogope kihivyo. Hapa kuna suala la elimu nadhani ni muhimu zaidi halafu ukiwa interested basi utanijia tuu inbox na au utazinunua nzitakapokufikia mahala ulipo.
 
Hili nililitarajia na nililiona pale tu nilipo maliza kusoma uzi wako.
Asante kwa huduma nzuri mkuu..[emoji4][emoji4]
Duh! Hapana usiogope kihivyo. Hapa kuna suala la elimu nadhani ni muhimu zaidi halafu ukiwa interested basi utanijia tuu inbox na au utazinunua nzitakapokufikia mahala ulipo.
 
Kwa mama mjamzito mbegu za maboga husaidiaa kuimarisha afya ya moyo na ini. Pia inachochea ukuaji na maendeleo bora ya afya ya ubongo ya mtoto. Mama Mjamzito anapokula mbegu za maboga anakuwa na uhakika wa kiwango stahili cha sukari kwenye damu (blood sugar level) na humuondolea maumivu ya tumbo na kuharisha
 
Mama anayenyonyesha anahitaji kuwa na mzaziwa ya kutosha. Inashauriwa kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo tangu kujifungua, mtoto anapaswa kunyonya maziwa ya mama pekee bila kuchanganyiwa na chakula kingine chochote.

matumizi ya mbegu za maziwa huongeza sana uzalishaji wa maziwa yenye afya yanayompa mama uhakika wa kunyonyesha ipasavyo bila kuteteleka.
 
Mtaua watu mara shia seed , mara mlonge seed, mara mwarobaini seed mtu mmoja dozi zote izo

Afu zote utasikia zinaleta hamu ya kula ,kuongeza nguvu ya kiume


If it isn’t perfect ,it’s not good enough
 
Tumia hata mtandao wa Google tuu kuyajua haya ni
Mtaua watu mara shia seed , mara mlonge seed, mara mwarobaini seed mtu mmoja dozi zote izo

Afu zote utasikia zinaleta hamu ya kula ,kuongeza nguvu ya kiume


If it isn’t perfect ,it’s not good enough
liyoyaandika. Ni tafiti zimebainisha haya. Halafu hizi ni njia za kuboresha afya zilizo salama kabisa kwa mlaji kwa kuwa haihusishi kemikali. Ni chakula cha asili ila kilicho tibalishe.
 
Back
Top Bottom