Zijue aina nne (4) za michepuko

vicarious

Senior Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
151
Reaction score
55
Zijue aina nne za michepuko:

1. MCHEPUKO LAMI
Huu ni ule ambao hauombi Pesa, katulia hana mapepe, uwe naye au usiwe naye maisha yake yanaendelea tu.

2. MCHEPUKO VUMBI
Huu ni ule wa vibomu mara sina pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa, oooh mara nipo saluni nadaiwa elf thelathin, naomba nauli. Na hii ndio noma maana njia kuu lazima washtuke mana mchepuko vumbi unachafua na unasumbua full time.

3. MCHEPUKO KOKOTO
Huu ni mkali zaidi ya njia kuu maana kila mara huuliza upo wapi, Uko na nani, why hupokei Simu yangu? Kama uko kwako naomba utoke nje tuongee kidogo na leo uwe na mimi tu,yaani tabu tupu.

4: MCHEPUKO GANZI
Yaani huu usiombe hata kukutana nao maana wenyewe ndio funga kazi. Huu bana unajua kuchuna hasa ila pale unapoupa pesa na wenyewe unaenda kuzihonga zote kwa mchepuko wake mwingine yaani hatari tupu.
 
hahahahha MUNGU NAOMBA NIPATE USINGIZI HAWA WATU WATAVUNJAA HIZI MBAVU
 
unachepuka wewe tena chepuko lako lina lami na bamsi huwek, zebra hakuna dah!! its dangerous

hahhhh sina chepuko sam love baibe wangu mmoja tu ningeekuwa na chepuko ningekuwa jf muda huu na wikiend hii hapa napoteza mawazo eti
 
Njia kuu zenyewe hazina vumbi na lami? 😀😱
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…