Zijue aina nne (4) za michepuko

......mchepuko kichakaaa.....
huuu hutakaa ujue wewe ni wa ngapi...kila mnyama apitae ataonja janiiiii na kujisitiri kivulini
 
Kuna mchepuko reli ya kati, njoo PM nikuelekeze
 
Kutoka njia kuu huenda kuna unalazima; nasema hivyo kwasababu siku zote njia kuu ni 01.Ila michepuko ipo 04;na michepuko hiyo ni kama ifuatavyo:-

1.MCHEPUKO LAMI
Yaani hapa ni raha kwenda mbele, hupati usumbufu.Nikimaanisha hakuna ooohhh nimeishiwa salio au uko wapi hivi sasa na unafanya nini.

Zaidi ya makubaliano na kufanya yenu kwa nafasi bila kukwazika kwa kupigwa mizinga na mambo kama hayo. Yaani hapa uwe naye usiwe naye yote sawa tu.Uwepo wenu ni pale mnapokubaliana jambo kwa muda fulani na linafanya kwa makubaliano bila hata kulalamika wala kulaumia.

2.MCHEPUKO VUMBI
Yaani hapa ni shida mwanzo-mwisho; yaani hakuna amani kabisa.Maana utasikia nirushie vocha, nitumie hela ya lunch basi,nitaka kuja ila sina nauli, mara baby sijaenda salon siku nyingi. Mara baby, ile simu yangu inazingua kweli yaani ninapata shida hebu nitafutie nyingine bwana. Yaani hapa ni fujo, isipokuwa makini hadi njia kuu anashitukia kuwa anachezewa foul.

3.MCHEPUKO KOKOTO
Yaani huu ni unakaba hadi penati; hapa huachiwi nafasi. Utasikia uko wapi saa hii, unafanya nini; mbona SMS yangu hujajibu? Halafu nilikuwa nakupigia simu naambiwa iko busy ulikuwa unaongea na nani? Ni mwanaume au mwanamke. Halafu unajua mimi sipendi hiyo tabia ya kuchelewa kupokea simu na kujibu sms zangu.
Yaani hapa, ni kama vile unakuwa umewekwa chini ya ulinzi.

4.MCHEPUKO GANZI
Yaani huu, unabembelezwa kama vile unapendwa sana. Lakini ukweli wake unakuwa unachunwa na kupigwa fix za hapa na pale.

Na mzigo unaohonga unaenda kuliwa na mwingine/wengine tu. Uki-mind unaishia kubembelezwa tu, utasikia baby usiwe na haraka mimi ni wako tu, yaani ungejua ninavyokupenda yaani usikasirike hivyo, sasa hasira za nini au ndiyo unataka kusema huniamini ama! Halafu ukimuhitaji mara utasikia ninajisikia vibaya, siku vizuri, niko msibani, niko hospital kuna ndugu yangu anaumwa. Usijali mtu wangu, nitakutafuta baadaye mara simu iliishiwa charge, nilikuwa sina salio, niliiacha kwenye charger.
 
Hahahaaaa Shida peleka kwako/kwenu michepuko matumizi tuuu hata huo wa lamii unatumia kikubwa maana lzm umtoe out ktk sehem za nguvuu,ukitaka kumwazima gari unawaza ulirudishe liko full tank na carwash limepita,shopng woolwoth nk. Ni shiiidaaa kote.
 
Umesahau moja, kuna njia kuu zingine hazina tofauti na michepuko yani full majanga kisa ana pete ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…