MsA11
JF-Expert Member
- Aug 15, 2017
- 303
- 582
ShukranInawezekana kwa sababu kwa kawaida watu wengi wa bara( wabara, ni neno la kiluguru/zaramo/kwere maana yake wa kuja, au asiye na asili na makabila ya pwani), walipokuja mikoa ya moro, pwani na dar ( jimbo la mashariki) waliweza kulowea na kuoa au kuolewa na kushindwa kurudi makwao ( mikoa ya tabora, mwanza, kigoma n.k) kwa hiyo wakafahamiana na watu wa pwani na wakahesabiwa kuwa miongoni mwa makabila haya ya pwani, kwa mfano leo hii kuna majina ya kina mganga uluguruni, ambayo kiasili ni kina maganga wa tabora. Kwahiyo kuna wa manyema, wanyamwezi, warundi,wakongo na makabila mengine mengi yaliyokuja pwani kama manamba au watumwa au wafanyabiashara, wakaishi kuoa na kuolewa na watu wa pwani na kizazi chao kikasahau asili ya kwao na kujitambulisha kama wazaramu au wakwere au waluguru. Yaani wamekuwa wazaramu kwa kuzaliwa au kutokujua asili ya kwao, ila chimbuko halisi la wazaramo ni uluguruni,na uziguani.Kwahiyo hao wa manyema walikuja na kuwakuta wenyeji ambao ni wazaramu,waluguru,wakwere,wandengereko, wakami, wakutu na wakakaribishwa na kuwa miongoni mwao, pia vizazi vyao vilijitanabaisha kama wazaramo. Kwahiyo wakawa wazaramu wa kuzaliwa….! Kimsingi hata mngoni ambaye atahamia ngerengere au tununguo au mlandizi, vizazi vyake baadaye vinaweza kujitambulisha kama kutoka kabila la wakwere/waluguru. Kwahiyo uhusiano ulipo ni kwamba, wa manyema walihamia maeneo ya pwani na kutekwa na utamaduni wa wenyeji, na kuwa wazaramu ila wazaramu si wa manyema na wala wa manyea si wazaramu.
Sent using Jamii Forums mobile app